Yapo maeneo kadhaa ambayo ni vivutio vya aina hii ya Utalii. Maeneo hayo ni pamoja na hifadhi ya asili ya Amani ambapo wanapatikana viumbe adimu ulimwenguni, vivutio vingine ni ufugaji wa vipepeo eneo la Amani, Maporomoko ya maji ya Mto Zigi, Ua la St Paulia, Mlima wa Mlinga, kanisa la kwanza la Angalican katika Tanzania- Utalii unajumuisha maeneo mazuri ya fukwe yaliyopo katika kata ya Kigombe. Uwekezaji katika sekta hii ni muhimu ili kukuza sekta ya utalii. Hii inajumuisha ujenzi wa hoteli za kitalii na ufugaji wa vipepeo.
1. Hifadhi ya asili ya Amani.
Hifadhi ya Asili ya Amani ilitangazwa kisheria na Serikali ya Tanzania katika Gazeti la serikali mwaka 1997, ikiwa na lengo la kuihifadhi bayoanuwai ya Milima ya Usamabara Mashariki. Safu ya Mashariki ya Milima ya Usambara imeorodheshwa kama kituo cha kimataifa cha bayoanuwai ya mimea na inajivunia kuwa ya pili kwa kuwa na aina nyingi za mimea katika bara la Afrika. Hifadhi hii ya viumbe hai yenye eneo la takribani hekta 83,600 inajumuisha misitu ya mvua na ardhi ya nyasi na miti ya uwanda wa chini. Ina sifa ya kuwa na mimea mingi iliyo katika hatari ya kutoweka (ikiwemo mimea mingi ya madawa) na ni makazi ya zaidi ya aina kumi na tatu za ndege wasiopatikana mahali pengine. Pia misitu hii mikuu hutoa maji kwa wakazi zaidi ya 300,000 katika mji wa Tanga, na wenyeji wa milimani wanategemea misitu hii kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaisha.
|
|
|
1.1 Watalii kutoka nchini Marekani wakifanya utalii
katika misitu ya Amani
|
1.2 Maporomoko ya maji katika mto Ziggi
|
2. MRADI WA UFUGAJI WA VIPEPEO AMANI
Wilaya ya Muheza katika msitu wa hifadhi wa Amani, kuna aina mbalimbali za vipepeo ambao kwa asili hawapatikani mahali pengine popote duniani. Njia nyingine mbadala ya kuendesha maisha kwa wakazi walioko katika milima ya Amani ni ufugaji wa vipepeo. Amani ina ushirikiano na shirika la madawa la ulaya ambalo hununua vipepeo wachanga, na kuwa chanzo kikubwa cha kipato kwa wakulima wenyeji.
Shughuli hizi za ufugaji wa vipepeo zimeanzishwa zikiwa na viwango mbalimbali vya mafanikio ya kupunguza athari za binadamu kwa mfumo wa ikolojia ya msitu, pasipo kuharibu bayoanuwai ya hifadhi
|
|
|
|
|
2.1 Kibanda maalum kwa ajili ya ufugaji wa vipepeo katika kijiji cha Fanusi wilaya ya Muheza.
|
|
2.2 Baadhi ya Aina za Vipepeo zinapopatikana Amani
|
Kusoma zaidi Fursa zote za Uwekezaji zinazopatikana katika Wilaya ya Muheza Tafadhari pakua hapa( fursa za uwekezaji MUHEZA.pdf) Na (SHUGHULI ZA UWEKEZAJI.pdf)
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.