Katika Wilaya ya Muheza shughuli za uvuvi zinafanyika katika bahari ya Hindi eneo la Kigombe. Uzalishaji wa samaki katika eneo hili ni mkubwa na unahitaji kuendelezwa. Uvuvi katika Wilaya ya Muheza unahusisha uvunaji wa samaki katika mabwawa, hivi sasa yapo mabwawa 84 yanayotumika kati ya mabwawa 128 yaliyopo. Hata hivyo ufugaji unaofanyika katika mabwawa kwa sasa ni kwa ajili ya matumizi ya chakula kwa mfugaji husika (Domestic use). Endapo mabwawa haya yataendelezwa uzalishaji wa samaki utaongezeka kwa kiasi kikubwa. Vichocheo katika uwekezaji huu ni kuwepo kwa miundombinu ya barabara (Barabara ya Tanga- Kigombe- Pangani), aina za samaki zilizopo na bwawa jipya la Misozwe ambayo yana nafasi kubwa ya uendelezaji.
Kusoma zaidi Fursa zote za Uwekezaji zinazopatikana katika Wilaya ya Muheza Tafadhari pakua hapa( fursa za uwekezaji MUHEZA.pdf) Na (SHUGHULI ZA UWEKEZAJI.pdf)
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.