Thamani ya mradi huu ni Tsh.166, 796,410. Mradi huu umekamilika kwa asilimia 100 na unaendelea kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Ubembe. Mradi una vituo kumi vya kuchotea maji.
Thamani ya mradi huu ni Tsh. 156, 349,707. Mradi huu umekamilika kwa asilimia 100 na unaendelea kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Kisiwani Nkumba. Mradi una vituo nane vya kuchotea maji
Mradi huu umekamilika kwa asilimia 100. Gharama ya mradi huu ni Tsh. 291, 500,000/=. Mradi una Tanki la kuhifadhia maji la juu ya ardhí lenye ujazo lita 45,000 na vituo vya kuchotea maji kumi na nne.
Thamani ya mradi huu ni Tsh. 224, 996,000/=Mradi huu una vituo vya kuchotea kumi, mfumo wa kuvuna maji ya mvua uliojengwa katika majengo ya shule na mfumo huo unahusisha wáter jar la ujazo wa Lita 1,000, fero cement ujazo wa lita 5,000, Tanki la plastiki lita 3,000 na una tanki la kuhifadhia maji juu ya ardhi la ukubwa wa lita 45,000.
Thamani ya mradi huu ni Tsh. 208, 720,600/= Mradi una vituo vya kuchotea kumi, mfumo wa kuvuna maji ya mvua uliojengwa katika majengo ya shule ya msingi Misongeni ambapo kuna wáter jar yenye ujazo wa lita 1,000, ferocement yenye ujazo wa lita 5,000, tank la plastic lenye ujazo wa lita 3,000 na tanki la kuhifadhia maji juu ya ardhi la ukubwa wa lita 45,000. Mradi huu umekamilika na unatoa huduma ya maji kwajamii.
Thamani ya mradi huu ni Tsh. 249,834,750/= Mradi una vituo vya kuchotea kumi na nne, mfumo wa kuvuna maji ya mvua uliojengwa katika kijiji cha Magila kutokana na kijiji kukosa majengo ya Taasisi kutokana na hilo miundombinu hiyo ya maji imejengwa katika eneo la zahanati ya Magila – kitako na tank la plastic lenye ujazo wa lita 3,000, wáter jar katika majengo ya shule ya msingi Magila na ferocement yenye ujazo wa lita 5,000 imejengwa katika majengo ya shule ya Sekondari Magila na tanki la kuhifadhia maji juu ya ardhi la ukubwa wa lita 45,000
Gharama ya mradi huu niTsh. 266, 167,000/=. Mradi huu chanzo chake cha maji ni kisima kirefu na utatumia mashine ya kusukuma maji kwa kutumia nguvu ya nishati umeme wa TANESCO hadi kwenye tanki lenye ukubwa wa lita 45,000 liliopo juu ya ardhi. Mradi una nyumba ya mitambo, kituo cha kunywea ng’ombe na mbuzi maji(cattle trough)vituo vya kuchotea vitano, mfumo wa kuvuna maji ya mvua uliojengwa katika eneo la shule ya msingi ambapo kuna tank la plastic lenye ujazo wa lita 3,000, water jar lita 1,000 na ferocement yenye ujazo wa lita 5,000.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.