Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mheshimiwa Ayubu Sebabili, leo tarehe 12/11/2025 amezindua Bodi Mpya ya Afya ya Wilaya, katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliyopo kata ya Lusanga.
Akizungumza wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa bodi hiyo, Mkuu wa Wilaya aliwapongeza wajumbe wapya ambao wanaanza muda wao, “Mimi nawapongeza kwa kuchaguliwa kwenu ni matumaini yetu kwamba mtaendeleza yale mazuri yote ya waliomaliza muda wao lakini pia kuleta chachu mpya ili kuhakikisha huduma za afya wilayani Muheza zinaendelea kukua”, alisema Mhe. Ayubu Sebabili
Aidha katika pongezi zake Mhe. Sebabili aliwapongeza wajumbe wa bodi waliomaliza muda wao kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kipindi chao katika usimamizi wa huduma za afya wilayani Muheza, ambapo moja kati ya kazi kubwa za kukumbukwa kwa bodi hiyo ni usimamizi wa ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya ya Samia.
Vilevile Mhe. Ayubu Sebabili aliwahakikishia wajumbe kua atawapa ushirikiano wakati wowote ule ambao watahitaji msaada, “Milango yangu ipo wazi mimi pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya muda wowote mkihitaji msaada wa hali na mali tutakua tayari kushirikiana nanyi hivyo msisite kutueleza changamoto zenu ili tuweze kuzipatia ufumbuzi kwa manufaa ya wananchi wetu Wikayni Muheza na taifa kwa ujumla”.
Bodi mpya imeanza majukumu yao leo mara baada ya uzinduzi ambapo inatarajiwa itakua ikifanya kazi hadi mwaka 2028
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.