Idara ya Maji ina jukumu la kutoa huduma ya maji safi na salama . Idara ina jumla ya watumishi 13 ambao ni wahandisi 2, mafundi sanifu 4, mafundi sanifu wasaidizi 7
Majukumu ya Idara ya Maji
1.Kupanga, kusimamia na kuratibu shughuli zote za miradi ya miundo mbinu ya maji ili kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa viwango vya ubora unaokubalika.
2.Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri wakati wa kuandaa na kutekeleza miradi ya ujenzi wa maji katika maeneo yote yanayotekelezwa miradi ya miundo mbinu.
3.Kusimamia utekelezaji wa sera, miongozo na sheria zinazotolewa na serikali juu ya utekelezaji na uendeshaji miradi ya maji ili iweze kuleta tija kwa kuinua uchumi na maendeleo kwa Taifa.
4.Kubuni na kusimamia miradi inayoanzishwa na jamii, Taasisi na Mashirika yasiyo ya kiserikali kwa njia shirikisha jamii kulingana na kanuni na miongozo inayotolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano.
5.Kufanya upimaji na uchunguzi wa miradi mipya ya maji.
6.Kusimamia uundaji wa vyombo vya watumiaji maji (COWSO).
7.Kusimamia sheria ya utunzaji wa vyanzo vya maji.
Idara ya maji inaundwa na Watumishi wafuatao
•Mhandisi wa maji Wilaya
•Mhandisiwa maji msaidizi
•Fundi Sanifu wanne
•Fundi Sanifu wasaidizi saba
Mgawanyo wa majukumu katika idara ni katika Tarafa
•Tarafa ya Muheza mjini inasimamiwa na Meneja maji Mjini na mafundi sanifu wawili
•Tarafa ya Ngomeni Fundi sanifu watatu
•Tarafa ya Amani Fundi sanifu watatu
•Tarafa ya Bwembwera fundi sanifu watatu
Idara inatoa huduma ya uchimbaji visima kwa kutumia mtambo wa Halmashauri na mpaka sasa Wilaya ya Muheza ina idadi ya visima 42 virefu na 86 visima vifupi na pia idara ya maji inatoa huduma ya kukodisha mtambo wa Halmashauri kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.