Mapema tarehe 21/11/2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Muheza Dr. Jumaa Mhina ameshiriki hafla fupi yakukabidhi ndoo na beseni kwa Waganga Wafawidhi wa vituo na zahanati arobaini na mbili (42) za Halmashuri ya Wilaya ya Muheza.
Hatua hii inakuja baada ya agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Nchemba alilolitoa tarehe 15/11/2025 jijini Dodoma katika hospitali ya rufaa ya mkoa, alipofanya ziara yakushtukiza, ambapo aliagiza hospitali zote nchini zihakikishe zinakua na vifaa vya usafi binafsi vya dharura vikiwemo ndoo na beseni katika wodi za wazazi ili ziweze kuwasaidia wakina mama watakaokua hawana vifaa hivyo.
Katika hafla hio fupi yamakabidhiano iliyofanyika katika chuo cha uuguzi cha St. Augustine Muheza Institute of Health and Allied Sciences (SAMIHAS) Dr. Mhina aliwataka watumishi hao kuvitunza vifaa hivyo nakuagiza kwamba wajawazito wote wanaofika vituoni wahudumiwe vizuri na isijekutokea mjamzito akakwamishwa kupewa huduma kwakukosa vifaa hivyo.
“Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi kwakushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya leo tunawakabidhi vifaa hivi vikatumike kwa kazi iliyokusudiwa yakuhakikisha wakina mama wajawazito wasiomudu kupata vifaa hivi wavipate vituoni kwenu kwa urahisi nakuhakikisha wanapata huduma zao bila adha zozote. Vilevile niagize yakwamba tusingependa kusikia mama mjamzito anashindwa kupatiwa huduma kisa hana vifaa, hivyo basi vikatumike kwa lengo lililokusidiwa” alisema Dr. Jumaa.
Zaidi Mkurugenzi Mtendaji alitoa wito kwa wadau mbalimbali wilayani Muheza kujitokeza na kuona wanawezaje kuchangia juhudi hizo na agizo la Waziri Mkuu kuhakikisha wakina mama Wilayani Muheza wanapata huduma bila adha zozote.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.