Maeneo yaliyotengwa Kwaajili ya uwekezaji katika Sekta mbalimbali
Wilaya ya Muheza ina mandhari, mazingira, fukwe za bahari, mila, desturi na tamaduni nzuri sana na zinazovutia kwa shughuli za kitalii lakini ina uhaba mkubwa sana wa miundombinu ya kitalii kama vile Hoteli na Nyumba za Kulala Wageni. Maeneo ya ujenzi wa miundombinu hiyo yapo katika maeneo yenye vivutio hivyo vya utalii.
Wilaya ya Muheza inakua kwa kasi kubwa sana kutokana na kuwa katika mazingira mazuri na yanayovutia watu wengi kuishi na kufanya kazi na biashara mbalimbali. Lakini wilaya kwa sasa haina huduma za miundombinu ya elimu ya kati na ya juu, yaani Ujenzi wa Vyuo vya Elimu ya Kati na Elimu ya Juu. Viwanja vya ujenzi wa miundombinu hiyo vipo tayari katika Eneo la Chatur na Muheza Estate na pia uwezekano wa kupatikana viwanja sehemu nyingine zaidi upo.
Sekta ya Afya ni moja ya sekta yenye hitajio kubwa sana kwa jamii. Mahitaji ya huduma bora za afya kila siku yamejuwa yakiongezeka. Vituo vya huduma za afya vilivyopo bado ni vichache na pia havikidhi mahitaji ya jamii. Maeneo ya kujenga miundombinu ya afya kama vile vituo Vituo vya Afya na Hospitali katika maeneo ya Chartur na Muheza Estate.
Wilaya ya Muheza haina kumbi za kisasa za mikutano na starehe na uhitaji wa huduma hizo kwa sasa ni mkubwa sana. Maeneo ya kujenga kumbi za kisasa za mikutano na starehe mbalimbali yapo.
Wilaya ya Muheza ni moja ya wilaya yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo kama vile matunda kama vile Machungwa, Maembe, na matunda mengine mbalimbali, Mihogo pamoja na mazao mengine ya aina mbalimbali. Kwa mantiki hiyo, kuna fursa kubwa sana ya kuwekeza katika viwanda vya uchakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo. Maeneo ya ujenzi wa viwanda hivyo yapo na pia uwezekasno wa kupata maeneo zaidi upo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.