TAARIFA YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
1.0 UTANGULIZI
Idara ya Maendeleo ya Jamii inahusika zaidi na kuraghibisha jamii ili iweze kushiriki kikamilifu katika Maendeleo,hii ni pamoja na kubadilisha,mitazamo,fikra,tabia,na mienendo ili iwe chanya kwaajili ya Maendeleo ya wananchi.
Kuiwezesha jamii kuibua kupanga na kutekeleza kwa kikamili yale waliyopanga kwa kutumia zaidi raslimali zilizopo maeneo yao na za nje pale zitakapohitajika
2.0 HALI YA WATUMISHI NA MUUNDO WA IDARA
Idara ya Maendeleo ya Jamii ina Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya na Maafisa Maendeleo watano 5 ngazi ya Wilaya na Maafisa Sita wako ngazi ya Kata
Idara ina madawati matano na Kitengo kimoja (1) kama ifuatavyo :
1.MADAWATI:
2.Utafiti na Mipango
3.Dawati la Jinsia na Watoto
4.Kikosi cha Ufundi na Ujenzi
5.Uwezeshaji wananchi kiuchumi
2.VITENGO
1.Idara ina Kitengo kimoja cha vijana
3.0 Pia Idara ina ratibu shughuli zifuatazo
1.Uratibu wa VICOBA
2.Uratibu wa shughuli wa TASAF
3.Uratibu wa Asasi
4.Uratibu wa Shughuli za Mwitiko wa Jamii katika kudhibiti UKIMWI
5.Uratibu wa Shughuli za Mradi wa ushauri wa kisheria kupitia mfuko wa ABBOT
4.0 MAJUKUMU YA IDARA :
1.Kuhamasisha na kuiwezesha jamii,kushiriki katika kutambua, kuibua, kupanga , kutekeleza, kufuatilia na kutathimini shughuli zao za Maendeleo.(To ensure that community Participate fully in formulating, Planning, implementing and evaluating Development Plans.
2.Kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli zote za Maendeleo ikiwemo miradi ya ujenzi ya kijamii,usafi wa mazingira
3.Kusimamia na kuhamasisha shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya uzalishaji mali vya wanawake ,vijana , vikundi vingine vya kiraia ,VICOBA na WEKEZA
4.Kuratibu shughuli za Mwitiko wa jamii katika kudhibiti UKIMWI
5.Kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora na uimarishaji wa vikosi vya ujenzi vya Kata vikiwemo vya vijana
6.Kuhamasisha shughuli zote za Maendeleo ya watoto .
7.Kukusanya takwimu mbalimbali za Maendeleo ya Jamii kwaajili ya Mipango ya Maendeleo ya jamii
8.Kuwezesha wanawake na vijana kuongeza kipato chao kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo, utoaji wa mikopo kwa vikundi vya uzalishaji mali vya wanawake na vijana kupitia mfuko wa Maendeleo wa Wanawake na vijana wa Halmashauri
9.Kuratibu shughuli zote za Asasi
10.Kuziwezesha jamii kutambua fursa walizonazo ili kutatua vikwazo vya maendeleo (mipango shirikishi).
11.Kujenga uwezo wa Halmashauri na vijiji juu ya utawala bora, upangaji mipango shirikishi na bajeti.
12.Kueleimisha jamii kuingiza masuala mtambuka katika mipango,bajeti, na shughuli za maendeleo kama usafi wa mazingira, mapambano dhidi ya UKIMWI, Mapambano dhidi ya rushwa na Jinsia
.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.