KITENGO CHA SHERIA
Kitengo cha sheria cha Halmashauri ya wilaya ya Muheza ni kati ya vitengo vyenye hadhi sawa na idara vilivyoundwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kikiwa na majukumu mbalimbali. Kitengo cha sheria kimeundwa na mkuu wa kitengo akisaidiwa na wanasheria wawili.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA SHERIA:-
1.Kutoa ushauri kwa masuala yote ya kisheria kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya na kwa wakuu wote wa idara (HODs)wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
2.Kuiwakilisha Halmashauri Mahakamani katika mashauri yote yanayoihusu Halmashauri kwa maana ya kushtaki au kushtakiwa.
3.Kufanya Mapitio ya Uhalali wa mikataba kwa mujibu wa sheria na kuandaa mikataba mbalimbali inayoihusu Halmashauri au Taasisi zake.
4.Kuandaa sheria ndogo za halmashauri na sheria ndogo za Vijiji vilivyoko ndani ya eneo la Halmashauri.
5.Kusimamia na kutoa mafunzo ya uendeshaji wa mabaraza ya kata wilayani Muheza.
6. Kuratibu na kusajili vyombo vya watumia maji wilayani Muheza.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.