Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mheshimiwa Ayubu Sebabili leo Novemba 12, katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Wilaya zilizopo kata ya Lusanga ameendesha kikao cha utekelezaji wa afua za lishe katika robo ya kwanza (July – Septemba) ya mwaka 2025-2026.
Katika taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe iliyosomwa na Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Fani Mussa alieleza kua hali ya utekelezaji wa afua hizo katika vigezo alama vyote kwa ngazi ya wilaya, kata na chama vyote vina alama ya kijani ambayo inaashiria wilaya imefanya vizuri.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya katika hotuba yake alipongeza huku akiwataka watu wote wanaotekeleza afua za lishe kuendelea kuongeza juhudi na kuhakikisha alama za kijani zinakua endelevu wakati wote na sehemu zinazotakiwa kuongezewa juhudi, kila mmoja aweke nguvu.
“Hongereni sana kwa kufanya kazi nzuri kwa kipindi hichi nakuhakikisha tunakua kwenye wastani mzuri wakijani, niwaombe muongeze juhudi hasa kwenye kuongeza mashine zenye uwezo wakuongeza virutubisho ziongezeke ili jamii na kwenye maeneo yetu watu waweze kupata virutubisho hivyo” alisema Mhe. Ayubu Sebabili.
Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi ngazi ya wilaya na halmashauri pamoja nawatendaji wa kata zote thelethini na saba (37) za halmashauri ya wilaya ya Muheza ambao ndio watekelezaji wakuu wa afua hizo katika ngazi ya jamii kwenye kata na vijiji vyao.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.