1. Utangulizi
Mazao ya kibiashara yanayolimwa Muheza ni kama machungwa, chai, mazao ya viungo ( iliki, mdalasini, pilipilimanga na karafuu) miwa, nazi, katani, kokoa na korosho. Uzalishaji wa mazao ya kibiashara kwa mazao 9 makuu katika muda wa miaka 4 mfululizo ni tani 111,154.85 kwa mwaka 2013/2014, tani 160,155.36 kwa mwaka 2014/2015, tani 261,363 kwa mwaka 2015/2016, na tani 272,204.6 kwa mwaka 2016/2017. Jedwali hapo chini laonesha.
Jedwali: Uzalishaji kwa tani kwa mwaka 2013/14 hadi 2016/17
Mazao
|
2013/14 |
2014/2015 |
2015/2016
|
2016/2017
|
|
Nazi
|
3,119.96 |
3,983.4 |
2,576
|
2,280.6 |
|
Mihogo
|
71,590 |
45,570 |
30,216
|
59,554.2
|
|
Machungwa
|
101,849.60 |
93,086 |
221,195
|
201,781.4
|
|
Korosho
|
229.2 |
98 |
215.6
|
199.2
|
|
Iliki
|
165.7 |
161.2 |
131.6
|
98.7
|
|
Mdalasini
|
198.5 |
232 |
105.2
|
202.6 |
|
Karafuu
|
380.6 |
487 |
392.6 |
432 |
|
Pilipilimanga
|
1032.19
|
1103.5
|
2123.3
|
2130.7
|
|
Chai (Wakulima wakubwa)
|
1,819 |
2,759 |
2123.3
|
1371.7
|
|
Chai (Wakulima wadogo)
|
136 |
134 |
134.5
|
151.2
|
|
Katani
|
2,224.1 |
2,614.26 |
2052.72
|
4099.7
|
|
Jumla Kuu |
111,154.85 |
160,155.36 |
261,363 |
272,204.6 |
|
|
2. Kilimo cha Mazao ya viungo(Mdalasini, Karafuu, Iliki, Pilipili Manga).
Uzalishaji na uuzaji wa viungo ni wa chini ingawa kuna maeneo mazuri ya uzalishaji. Kuna ukuaji mkubwa wa mahitaji ya mazao ya viungo duniani ikiwa uzalishaji utakuwa na ubora hasa kilimo kisichotumia mbolea za viwandani. Soko la nje ni kama Afrika ya kati, Asia, Ulaya, Afrika na Amerika. Soko la ndani linajumuisha Zanzibar na Tanzania Bara. Hivyo wanadau mbalimbali wanakaribishwa katika uwekezaji wa mazao ya viungo hasa kwenye uzalishaji na uongezaji thamani ( usindikaji wa viungo).
|
|
|
|
|
|
1. Pichani ni Mazao ya viungo kushoto Karafuu, Katikati ni Iliki, na kulia ni Pilipilimanga, Mdalasini (nyuma). |
|
2. Pilipilimanga katika hali ya ubichi (chini)
|
|
3. Shamba la chai Amani
|
|
3. Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika Sekta ya KIlimo;
Shamba lina ukubwa wa Hekta 3,036.36 na limepimwa, eneo la ardhi lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji ni Hekta 892.1 na utaratibu wa uwekezaji utakaotumika ni ubia au Kuuza.
Viungo vinavyostawi katika Wilaya ya Muheza ni Iliki, Mdalasini, Karafuu, Pilipili manga na Kakao. Uzalishaji na uuzaji wa viungo ni wa chini ingawa kuna maeneo mazuri ya uzalishaji. Kuna ukuaji mkubwa wa mahitaji ya mazao ya viungo duniani ikiwa uzalishaji utakuwa na ubora hasa kilimo kisichotumia mbolea za viwandani. Soko la nje ni kama Afrika ya kati, Asia, Ulaya, Afrika na Amerika. Soko la ndani linajumuisha Zanzibar na Tanzania Bara.
Eneo lililotengwa ni Kihuhwi shamba la Bwembwera lenye ukubwa wa hekta 2,300. Uzalishaji wa mpira kibiashara bado haujaendelezwa hapa Tanzania kiujumla, Uzalishaji wa Mpira katika Tarafa ya Bwembwera ni mkubwa na kama utaendelezwa bidhaa nyingi zinazotokana na mpira zitazalishwa.
Kusoma zaidi Fursa zote za Uwekezaji zinazopatikana katika Wilaya ya Muheza Tafadhari pakua hapa( fursa za uwekezaji MUHEZA.pdf) Na (SHUGHULI ZA UWEKEZAJI.pdf)
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.