Kitengo cha ukaguzi wa ndani kimeanzishwa kisheria chini ya kifungu namba 45 cha sheria ya fedha ya serikali za mitaa ya mwaka 1982.
Majukumu ya kitengo cha ukaguzi
1.Kukagua na kuripoti mfumo mzima wa mapato wa Halmashuri na udhibiti wake
2.Kusimamia kama Halmashauri inazingitia sera, kanuni, taratibu na sheria katika utekelezaji majukumu yake
3.Kuhakiki uhalisia na ubora wa taarifa fedha na miradi zinazotolewa na wakuu wa idara katika maandalizi ya vitabu vyama hesabu vya Halmashauri
4.Kuhakiki ubora na taratibu nzima za utunzaji mali za Halmashauri
5.Kuhakiki uwajibikaji wa Halmashauri na kuhakikisha malengo ya Halmashauri yanafikiwa.
6.Kuhakiki na kufuatilia majibu ya hoja za ukaguzi wa ndani na nje yanajibiwa kwa wakati pamoja na ushauri uliotolewa na wakaguziu mezingatiwa na kutekelezwa.
7.Kufanya ukaguzi wa nyaraka na miradi na kutoa taarifa ya matokeo ya ukaguzi huo
IDADI YA WATUMISHI KATIKA KITENGO CHA UKAGUZI
a)Kaimu Mkaguzi wa Ndani
b)Mkaguzi wa ndani II - 1
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.