Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Muheza ulianza mnamo tarehe 28/12/2017 kwa kutumia mafundi wa kawaida(Local contractor). Mradi huu unategemewa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2017/2018 hadi 2019/2020 itategemea upatikanaji wa fedha , Aidha mradi huu utategemea Nguvu za wananchi, Wadau mbalimbali na serikali.
Mradi huu utagharimu jumla ya TZS 11,322,459,300 aidha mradi utatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza itahusisha majengo ya utawala, wodi ya wanawake, wodi ya watoto, jengo la upasuaji, jengo la maabara, jengo la utakasaji vifaa na jengo la dharura ambayo yatagharimu TZS 3,899,759,100.
Halmashuri ya Wilaya Muheza imetenga 150,000,000 kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali kuu imetenga TZS 1, 500,000,000. Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya kuendeleza mradi, hivi karibuni Halmashauri imepokea kiasi cha TZS 500,000,000 kutoka serikali kuu.
Kambi ya vijana CCM Mkoa wa Tanga wakisaidia kumwaga zege la jamvi katika ujenzi wa Hospitali ya wilaya mnamo Tarehe 18/09/2018 |
|
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe, Abdallah Ulege akisaidia kupandisha kuta za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Muheza. |
|
||
|
HATUA ILIPOFIKIA
Mpaka sasa hatua iliopo ni ujenzi wa kuta
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.