Mratibu wa Zoezi la Sensa ya watu na Makazi Wilaya ya Muheza ambaye pia ni Afisa takwimu wa Wilaya hiyo amesema Wilaya ya Muheza katika Zoezi la Sensa ya watu na makazi imefikia asilimia 91.36 tangu zoezi hilo la kuhesabu watu lilipoanza mnamo mwezi Agosti 23, 2022 Nchi nzima.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walipofika ofisini kwake mapema leo tarehe 1/9/2022.
Aliendelea kueleza kuwa katika Sensa ya Mwaka huu wa 2022 Wilaya ya Muheza ilikisia kuandikisha kaya 71,735 lakini mpaka sasa imefikia kaya 65,537 ambayo ni sawa na asilimia 91.36 ya lengo la kaya zilizotakiwa kufikiwa.
Ametoa rai kwa wananchi ambao mpaka sasa hawajahesabiwa watoe taarifa kwa wenyeviti wa vitongoji, na ofisi ya Mratibu wa Sensa Wilaya ya Muheza ili waweze kuhesabiwa na kutimiza adhima ya Serikali.
“Niwasihi wananchi ambao hawajahesabiwa taarifa zitolewe kwa wenyeviti vitongoji waratibu wa sensa waliopo kwenye maeneo yenu watu wote wahesabiwe, tuko tayari kukufuata eneo lolote ulipo ili kuweza kutimiza lengo la Serikali” alisema Mwankina.
Aliongeza kuwa zoezi la kuhesabu watu limeongezwa siku saba (7) ambazo zimeanza tarehe 30/8/2022 na litakwisha tarehe 5/9/2022 ili kutoa fursa kwa wananchi ambao walikuwa hawajafikiwa na zoezi hili waweze kuhesabiwa katika kipindi hicho.
Aidha katika zoezi la kuhesabu na kusajili majengo lililoanza rasmi tarehe 30/8/2022 hadi kufikia tarehe 31/8/2022 jumla ya Majengo 70,733 Wilayani Muheza yamefikiwa na kusajiliwa.
“SENSA KWA MAENDELEO JIANDAE KUHESABIWA KWA MAENDELEO YA TAIFA”
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.