Shirika la World Vision Tanzania limetoa msaada wa Examination gloves,Face Mask Surgical na vitakasa Mikono kwa Halmashauri ya Wilaya Muheza kuunga mkono Serikali katika jitihada zake za kupambana na Ugonjwa wa homa ya Mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.
Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika mnamo siku ya Ijumaa tarehe 15/5/2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiwemo wakuu wa Idara na Vitengo.
Akisoma taarifa ya Makabidhiano Mshauri wa Masuala Afya na Lishe Taasisi ya World Vision kanda ya Mashariki ANDREAS MTITA amesema Shirika linakabidhi vifaa kadhaa vyenye thamani ya Shilingi 14,655,000/= vitakavyosaidia kujikinga na maambukizi hayo ambapo vifaa vya shilingi 9,755,000/=vinakabidhiwa siku hiyo ikiwa vifaa vyenye thamani ya shilingi 4,900,000/= vitakabidhiwa baada ya wiki mbili.
Aliendelea kuwa vifaa vilivyokabidhiwa siku hiyo ni Chroline tab 30 , barakoa 3000. Sanitizers 15 , Sabuni ya maji lita 15, Spirit lita 15, na Examination gloves box 10 na vifaa vinavyotarajiwa kukabidhiwa ni infrared thermometer 5, Face Mask N95 200 na examination gloves 100.
Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe Mhandisi MwanashaRajab Tumbo ameshukuru taasisi hiyo kwa upendo waliouoneshsa katika wilaya Muheza na kutoa wito kwa Wadau wengine waweze kujitoa kama WORD VISION walivyojioa ili kupambana na janga hili la Corona.
Aliongeza kuwa kwa kuwa siku ya tarehe 15/5/ ni siku ya siku ya familia amewataka wajumbe wote waliohudhuria katika hafla hiyo kuchukua nafasikwenda kuzungumza na familia namna ya kukabiliana na tatizo la Corona kwa kufanya akiwa na imani kuwa ndio mbinu pekee itakopelekea kutoenea kwa urahisi kwa ugonjwa huu.
“sisi tuliopo hapa ni mabalozi tukatoe elimu majumbani mwetu, katika familia zetu , tukatoe elimu kwa wenzetu ili kusaidia kutokomeza janga hili” alisema Mhe Mkuu wa Wilaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Nassib Mbagga ameipongeza Taasisi ya WORLD VISION kwa jitihada walizozionyesha kwani amekuwa akiumiza kichwa kila siku namna ya kupata vifaa japo vichache tu ili kuweza kupambana na ugonjwa huu.
Pia alimshukuru mkuu wa Wilaya hiyo Mhe, Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo kwa kuwa Mstari wa mbele kwani amekuwa akimpa ushirikiano mzuri na wa karibu zaidi wakati anapokuwa akihitaji msaada toka kwake.
|
|
|
---|---|---|
VIONGOZI WA MUHEZA WAKISUBIRI KUKABIDHIWA VIFAA | VIFAA VILIVYOKABIDHIWA MUHEZA NA SHIRIKA LA WORLD VISION. | MKUU WA WILAYA AKIKABIDHI BANGO LA HATUA ZA UNAWAJI ILI KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA |
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA NASSIB MMBAGGA (MWENYE SUTI YA KIJIVU) NA MKUU WA WA WILAYA MUHEZA MHE, MWANASHA RAJAB TUMBO MWENYE HIJJAB NYEUSI WAKISUBIRI KUPOKEA MSAADA WA VITAKASA MIKONO KUTOKA KWA TAASISI YA WORLD VISON
|
MGANGA MKUU WILAYA MUHEZA DKT FLORA KESSY (ALIESIMAMA) AKIZUNGUMZA KABLA YA MAKABIDHIANO YA VIFAA HIVYO YALIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO HALMASHAURI | MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA MUHEZA (WA KWANZA KUSHOTO) AKISHUHUDIA MAKABIDHIANO YA BANGO LA HATUA ZA UNAWAJI MIKONO ZA KUJIKINGA NA CORONA KATI YA MKUU WA WILAYA MUHEZA (MWENYE HIJJABU NYEUSI) NA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA WORLD VISION KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI.. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.