Shirika lisilo la kiserikali World vision lenye makao makuu Hale Wilayani korogwe imeamua kufanya mafunzo kwa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ngazi ya Wilaya baada ya kuona vitendo hivyo kuongezeka katika jamii.
Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya Muheza jana Muwezeshaji wa mradi World Vision Ndugu Akilimali Yohana Leverian amesem a lengo la mafunzo ni kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto unasimamiwa ipasavyo katika jamii hivyo basi jukumu la kumlinda mtoto ni la mzazi/mlezi, serikali ya jamii yote inayomzunguka mtoto.
Pia aliitaka kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ngazi ya wilaya ikasaidie kuunda kamati ngazi ya kata na vijiji na ikatoe mafunzo stahiki kwa jamii hivyo basi ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukomeshwe.
Akielezea dalili za mwanamke au mtoto aliefanyiwa ukatili Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Tanga (muwezeshaji) Ndugu Emily Mashauri alisema mtoto au mwanamke aliefanyiwa ukatili huwa mnyonge,hukosa amani, hajiamini, huishi kwa kujitenga na hali chakula vizuri.
Pia Afisa Ustawi wa jamii Mkoa Tanga(muwezeshaji ) Ndugu Mmassa Malugu ameeleze kuhusu malezi, msaada na uhusiano katika jamii kuwa, Malezi ni utoaji wa huduma muhimu kwa mtoto zikiwemo, ulinzi, afya elimu na uchangamshi.
Aliongeza kuwa kabla mtoto kuzaliwa mama anahitaji kuhudhuria kliniki mara nne kwa ajili ya kupata chanjo za kumkinga mtoto aliopo tumboni na mtoto azaliwapo apewe chanjo ya pepopunda ili kumkinga na ulemavu “huduma muhimu za malezi baada ya kuzaliwa mtoto ni chanjo nyingine kama kifua kikuu, kifadulo, polio, donda koo, pepopunda, homa ya ini na homa ya uti wa mgongo ambazo humkinga na magonjwa ya mlipuko” alisema Mmassa.
Katika upande wa lishe malugu amesema kuwa mtoto anahitaji lishe bora na kunyonya maziwa ya mama katika kipindi cha mwaka mmoja ilia pate viini lishe muhimu kutoka mwilini. Mtoto anatakiwa kula mlo kamili kwa maana ya makundi matano ya vyakula vyenye Wanga, Vitamin, Protini, Madini na kimiminika.
Akizungumzia ulinzi na usalama wa mtoto alisema mtoto anatakiwa kulindwa dhidi ya aina zote za ukatili kama ukatili wa kimwili(kupigwa, kubakwa, kulawitiwa) kisaikolojia na kiakilli kwani watoto wana haki ya kusikiliza na kushirikishwa katika Nyanja zote za maendeleo katika maisha yao hivyo basi amewataka wazazi/walezi kuwa na urafiki na watoto ili wawe huru na wanachotaka kuongea.
Akitoa neo la ushirikiano, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bwana Godhelp Ringo amesema halmashauri iko tayari kushirikiana na World Vision kwa kuwaruhusu watumishi kufanya nao kazi ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na akasisitiza kuwa mafunzo yawe endelevu ili wanakamati waendelee kuwa na uelewa zaidi.
Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Wilaya Muheza Ndugu Desteria Haule, alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kuingiza bajeti ya kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Mpango wa bajeti ya mwaka 2019/2020 na mpango huo upite kwenye vikao vyote, pia ameitaka jamii kutokomeza mila na desturi potofu kama za kukeketa mwanamke, kuwe na haki sawa kwa
wanakamati wakimsikiliza muwasilisha mada kwa makini |
|
wanakamati wakijibu maswali |
---|---|---|
|
||
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.