Waziri wa Tamisemi mhe, Selemani Jaffo atembelea wilaya Muheza katika miradi ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya uliopo Lusanga na ujenzi wa mabweni ya watoto wenye mahitaji uliopo katika kata ya Mbaramo maalum leo tarehe 31/1/2019 ili kujiridhisha na utekelezaji wa miradi hiyo.
Akitembelea katika mradi wa ujenzi wa Hospitali Wilaya, Jaffo amesema Serikali imetenga kiasi cha TZS bilioni 1.5 kwa ajili ya kusaidia katika ujenzi huo na kuagiza kuwa mnamo tarehe 15/12/2018 kila Halmashauri iwe imeanza ujenzi na iwapo haitokuwa imeanza pesa zitahamishwa kupelekwa Halmashauri nyingine lakini amewapongeza viongozi wa muheza kwa hatua waliofikia.
Aidha amewataka viongozi wa wilaya kushirikiana kwa pamoja kusimamia ujenzi huo na kuwashauri waongeze mafundi kwani majengo 7 ni mengi inatakiwa kila jengo liwe na mafundi wake ili kazi iweze kukamilika kwa wakati ambapo mpaka tarehe 30/6/2019 hospital inatakiwa iwe imekamilika. “lengo la serikali ni kuona wananchi wanapata Hospitali ya Wilaya”alisema Jaffo
Kwa upande mwingine ametembelea mradi wa ujenzi wa mabweni ya watoto wenye mahitaji maalum uliopo katika kata ya Mbaramo ambako aliwashukuru wananchi kwa kujitoa nguvu zao kwani wanjua umuhimu wa elimu “ukiona jamii imeamua kutoa nguvu zao ni jambo la msingi sana “alisema Selemani
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.