Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Ayubu Sebabili amewataka Wananchi wa Wilaya hiyo kutoa taarifa za wanaotishia kuvunja Amani kwenye vyombo vya Usalama katika kipindi hiki cha Kuelekea siku ya kupika Kura inayotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 kwa ajili ya kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Wito huo ameutoa mapema siku ya Jumamosi Oktoba 18, 2025 alipokuwa Mgeni rasmi katika Bonanza la Michezo (Jogging) lililofanyika kuanzia Uwanaja wa Jitegemee na kukimbia kuelekea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Muheza.
Matembezi hayo ya Amani yalihusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, Watumishi wa Halmashauri, watumishi wa taasisi mbalimbali zilizopo Wilayani hapo, Klabu ya Jogging ya Jiji, Muheza na wananchi.
Akizungumza mara baada ya Mazoezi hayo Mkuu huyo wa Wilaya ya Muheza amesema lengo la Bonanza hilo ni kuhamasisha wananchi kwenda kupiga Kura siku ya Jumatano tarehe 29/10/2025 kwa Amani na Utulivu.
“Nitoe wito kwa wananchi wenzangu wa Wilaya ya Muheza kuhakikisha tunatoa ushirikiano kwa Vyombo vyetu vya ulinzi pindi tutakapoona watu wenye nia ovu wanaleta Uchochezi unaolenga kukataza au kuhamasisha watu kuvuruga zoezi la Uchaguzi katika kipindi hiki cha chote hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, vyombo viko imara na viko tayari kumshughulikia yeyote anaetaka kuvuruga Amani ya Nchi” alisema Mhe. Sebabili.
Kwa Upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza Ndg Serapion Bashange amewataka wananchi kutompatia mtu yeyote kazi zao za kupigia Kura ili waweze kutimiza haki na wajibu wao wa kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka na watakaowaletea maendeleo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wananchi wa Wilaya hiyo, Peris Kilima, Mukadam sabuni na Sudi Mohamed wamesema wamehamasika kwenda kupiga kura kwa ajili kuchagua viongozi watakawaoongoza katika kipindi kingine cha Miaka 5 (2025-2030).
| DC SEBABILI AKIHUTUBIA |
|
DC SEBABILI AKIONGOZI MBIO |
|
DC AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA |
|
|
![]() |
|
![]() |
|
![]() |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
![]() |
|
![]() |
|
![]() |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
![]() |
|
![]() |
|
![]() |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.