Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa leo tarehe 16/10/2025 amekuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa imefanyika Mkoani Tanga kuanzia tarehe 10 hadi leo ambapo yamehimishwa katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara.
Katika hotuba yake Mheshimiwa Majaliwa amesema kua Serikali inahakikisha Tanzania inaendelea kuwa kitovu cha Uzalishaji wa chakula wa chakula katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki kwa kuendelea kufanya mageuzi katika Sekta ya Kilimo.
“Kuna ongezeko kubwa katika uzalishaji wa mazao ya chakula kufikia tani Milioni 22 kwa Mwaka 2023/2024 ukilinganisha na tani Milioni 18 Mwaka 2020/2021 na Kiwango cha utoshelevu wa Chakula kuongezeka kutoka asilimia 114 hadi 128 Mwaka 2024/2025”.
Aidha Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakulima wote nchini wafugaji pamoja na wavuvi kuongeza thamani ya mazao yao kwa kusindika na kuongeza ubunifu.
Maadhimisho hayo yamedumu kwa wiki moja Jijini Tanga yalikua yakiongozwa na kaulimbiu isemayo, “Tuungane pamoja kupata chakula Bora kwa Maisha Bora ya Baadae”.
|
|
|
|
|
|
|
![]() |
|
![]() |
|
![]() |
![]() |
|
|
|
|
|
|
|
![]() |
|
![]() |
|
![]() |
![]() |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.