Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na watoto Mhe Ummy Mwalimu amezindua Wiki ya Unyonyeshaji kitaifa uliyofanyika tarehe 1/8/2020 katika Uwanja wa Jitegemee Wilayani Muheza.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji ya Mwaka 2020, “Tuwawezeshe Wanawake kunyonyesha Watoto kwa Afya Bora na Ulinzi wa Mazingira” ikiwa na maana kuwa unyonyeshaji wa Maziwa ya mama ni suluhisho mojawapo ambalo linahitaji ushiriki mkubwa wa sekta mbalimbali ili kutatua changamoto za kiafya na kimazingira.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe Ummy amesema Maziwa ya mama ni muhimu katika ulinzi wa afya ya mtoto kwa kuwa humsaidia kukua vizuri, kuwa na uelewa wa haraka Shuleni pia humuepusha na magonjwa ya mara kwa mara.
Aliongeza kuwa Unyonyeshaji watoto maziwa ya mama hupunguza kiwango cha matumizi ya maziwa na vyakula mbadala vya watoto wachanga na wadogo yanakwenda sanjari na matumizi ya vifungashio mbalimbali vya plastiki, nishati kama kuni, mkaa na chupa za kulishia watoto ambavyo huchangia ongezeko la hewa ya ukaa (kaboni) inayoathiri mazingira ya dunia.
Katika hatua nyingine amekabidhi vitini vya lishe ya wanawake, watoto na vijana balehe kwa ajili ya vyombo vya habari ili elimu ya lishe iweze kusambazwa katika jamii hatimaye kuchochea mabadiliko chanya ya tabia zinazoathiri lishe.
Aidha amewataka wakina mama kuwanyonyesha watoto wao miezi 6 mfululizo bila kuwapatia kupewa kinywaji au chakula kingine chochote ili kuboresha hali ya lishe ya mtoto aweze kukua vizuri kimwili na kiakili.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe Mwanasha Rajab Tumbo amewataka wakina mama wanyonyeshe watoto kwa kuwa ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango.
MHE UMMY MWALIMU ( WA KATIKATI) AKIINGIA UWANJANI JITEGEMEE MARA BAADA YA KUWASILI MUHEZA. | MHE, UMMY MWALIMU (MWENYE NGUO ZA VITENGE) AKISALIMIANA NA MKUU WA WILAYA MUHEZA MWENYE HIJABU NYEUSI PAMOJA NA VIONGOZI WA KAMATI YA CHMT |
|
|
|
|
|
|
||||
|
|
||||
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.