Katibu Tawala Wilaya Muheza Desderia Haule ambae alikuwa Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Mwanasha Rajabu Tumbo katika Uzinduzi wa Mpango wa Kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye Umri Chini ya Miaka mitano amewataka wazazi kuwasajili watoto hao kwenye mpango huo ili kuwaepusha na usumbufu pindi wasajiliwapo shuleni.
Akizungumza katika Hafla hiyo iliyofanyika mnamo tarehe 6/8/2020 kwenye Kitongoji cha Majengo kata ya Majengo (Nje ya Benki ya CRDB) Bi. Desderia amesema cheti cha kuzaliwa humsaidi mtoto kutambulika pamoja na wazazi wake kisheria hali inayopelekea kupata msaada wakati apatapo matatizo.
Aliongeza kuwa cheti cha husaidia kupata hati ya kusafiria nje ya Nchi hivyo basi kumuwezesha mtu kujulikana kwamba ni raia wa Nchi gani
Alisisitiza kuwa cheti hiki humuwezesha Mwanafunzi kujiunga na Vyuo na mikopo ya Elimu ya juu ikiwa na maana kuwa kila Mwanafunzi anaetaka kujiunga na shule ya Msingi, Sekondari na Chuo Kikuu ni Lazima awe na Cheti cha kuzaliwa hivyo.
Akiendelea kuzitaja faida za cheti cha kuzaliwa, Katibu tawala Wilaya Muheza amesema husaidia kupata ajira Taasisi za Serikali na Majeshi ya Ulinzi na Usalama ili kumwezesha mwajiri kutambua umri halali wa Mwajiriwa wake itakaomsaidia kujua kama anastahili kuajiriwa au hastahili kulingana na vigezo alivyoviweka.
Vile vile cheti cha kuzaliwa ni kitambulisho cha msingi ili kupata kitambulisho cha Taifa kinachomwezesha mtu kupata mkopo, dhamana katika sehemu yoyote ile nchini.
Aidha amewataka vyombo vya ulinzi na Usalama kuwachukulia hatua wasajili/ waandikishaji watakaobainika wamepokea rushwa katika zoezi hili ikiwa cheti cha kuzaliwa hutolewa bila malipo.
“Nitoe wito kwa waandikishaji wa zoezi hili kuwa mnatakiwa kuwa waadilifu kama mlivyoelekezwa katika mafunzo yenu , na mfahamu kuwa vyombo vya usalama vinawamurika popote mlipo atakaekwenda kinyume na taratibu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake: alisema Bi Haule.
Awali akisoma hotuba ya uzinduzi wa mpango wa kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya Miaka mitano Afisa ustawi wa jamii Wilaya Muheza Bi KIBBAH ANYANDWILE amesema mpango huu umebuniwa na Serikali kupitia Wakala wa Usajili na Ufilisi na Udhamini (RITA) kutokana na idadi kubwa ya wananchi kutosajiliwa hivyo kupelekea kuwa na idadi ndogo ya watu wenye vyeti vya kuzaliwa.
Amesema kwa mujibu wa takwimu ya ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 201 ni asilimia 13.4 tu ya wananchi wa Tanzania bara wamesajiliwa na wana vyeti vya kuzaliwa hivyo basi Serikali Awamu ya Tano inayoongozwa na DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI imeamua kuwasogezea karibu wananchi wake huduma hii hivyo wajitokeze kwa wingi.
Akivitaja vituo vya kutolea huduma hii Kibbah amesema vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano hutolewa katika OFISI ZA WATENDAJI KATA na vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya afya ya mama na mtoto.
Alisema kuwa taarifa za mtoto huingizwa kwenye simu na kuzisafirisha kwenda katika kanzi data ya RITA hivyo kusaidia utunzaji (archiving) na upatikanaji (retrieval) wa kumbukumbu kuwa na ufanisi zaidi.
Aidha Halmashauri ya Wilaya Muheza inatarajia kusajili watoto 32,038 walio na umri chini ya miaka mitano na hawana vyeti vya kuzaliwa hivyo basi wanachi wajitokeze kwa wingi kwani zoezi hili linatakiwa kukamilika ndani ya kipindi cha wiki mbili na baada ya hapo mfumo utaendelea katika vituo vya tiba ambapo kila mtoto atakaezaliwa atapata cheti cha kuzaliwa ndani ya muda mfupi.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
PICHANI NI WAZAZI WALIOHUDHURIA KWENYE UZINDUZI WA USAJILI NA UTOJI VYETI KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO ULIOPO KATA YA MAJENGO TAREHE 6/8/2020. | KAIMU MKURUGENZI WILAYA MUHEZA AMBAE NI AFISA UTUMISHI WA WILAYA HIYO AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI. | AFISA MAENDELEO YA JAMII (WA PILI KUSHOTO) BI POTINA GUGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI NA (WAKWANZA KUSHOTO) NI AFISA USTAWI WA JAMII AMBAE NI MRATIBU WA ZOEZI LA USAJILI NA UTOAJI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO HAO. | MGANGA MKUU WILAYA MUHEZA DKT FLORA KESSY AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI, ALIEVAA NGUO ZA VITENGE NI KATIBU TAWALA WILAYA MUHEZA BI DESDERIA HAULE AMBAE AMEMWAKILISHA MKUU WA WILAYA MUHEZA MHANDISI MWANASHA TUMBO KWENYE UZINDUZI HUO. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.