Wazazi wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawapatia watoto haki zao za msingi ili waweze kujenga na kuinua uchumi wa familia zao na Taifa kwa kuwa aTaifa linawategemea na kuamini kuwa wao ndio viongozi wa baadae.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Mwakiishi wa Mkuu wa Wilaya Muheza ambaye ni mgeni rasmi katika hafla hiyo Katibu Tawala Wilaya ya Muheza Desderia Haule amesema wazazi wanatakiwa kuhakikisha watoto wanawapeleka watoto shuleni wakapate elimu ilwaweze kuwa viongozi wa Taifa hili
Aliendelea kuwa ulinzi wa mtoto ni jukumu la mzazi/mlezi hivyo basi kila mzazi/mlezi ahakikishe mtoto wake haendi kwenye vigodoro usiku il kumlinda na vitendo vya ukatili vinavyoweza kujitokeza akiwa mahali hapo kama vile ubakaji, ulawiti na kumuepusha mimba za utotoni ambavyo vinaweza kufifilisha ndoto zao.
“Viongozi wa Serikali, na wadau wengine tuwe mstari wa mbele kutetea haki za mtoto , nanyi watoto mtoe taarifa kwa wazazi/ walezi na walimu ukiona mwenzio au wewe mwenyewe anafanyiwa ukatili, tusiwaruhusu watoto kwenda kwenye kumbi za starehe usiku” alisema Bi Desderia.
Awali akielezea historia ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye ni Afisa maendeleo ya jamii wilaya Muheza Bi. Vije Mfaume Ndwanga amesema imetokana na wanafunzi ,2,000 waliouwawa huko SOWETO Afrika kusini Mwaka 1976 walipokuwa wakiandamana ili wapate haki zao za msingi na kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwa ukifanywa utawala wa makaburu.
Akizungumzia haki ya mtoto ya kupata lishe bora Afisa maendeleo ya jamii Potina Guga amesema lishe ya mtoto huanzia tangu mimba inapotungwa tumboni ambapo mtoto anatakiwa kupata makundi 5 ya vyakula, Nafaka kama vile mchele, mahindi na mhogo, vyakula vya nyama maziwa, matunda ya aina yote, mbogamboga kama mchicha spinachi na mafuta na asali ili kuwaepusha na udumavu kwani mtoto akipata mlo kamili humsaidia kuwa msikivu na mbunifu shuleni na mwenye kufanya vizuri darasani.
Vile vile mada mbalimbali za lishe, haki za mtoto, sheria ya mtoto,, madawa ya kulevya na madhara yake viliwasili, ukatili viliwasilishwa ili kumlinda mtoto na asiweze kupoteza ndoto zake za baadae.
Katika htukio jingine mgeni rasmi Desderia Haule alitoa vyeti 16 kwa wanafunzi waliofaulu vizuri darasani wa shule ya msingiubembe, Nkumba, Nkumba kisiwani na Matombo
Aidha hafla hii ilihudhuriwa na wanafunzi 600 wa shule ya msingi, ubembe, Nkumba, Nkumba kisiwani, Matombo na shule ya sekondari Nkumba pamoja na viongozi wa siasa, viongozi wa dini kiislam na kikristo, wadau, WORLD VISION, LUNGUZA, MKUTA, ZICOSAD, SHIDEPHA, NMB, CRDB ZICOSAD, NA WATUMISHI WA HALMASHAURI MUHEZA NA WANANCHI.
KATIBU TAWALA WILAYA MUHEZA AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAADHIMISHO | KATIBU TAWALA WILAYA YA MUHEZA DESDERIA HAULE AKITOA ZAWADI KWA WATOTO 16 WALIOFAUKU VIZURI. | DIWANI KATA YA MAJENGO MHE, MUKADAM ABASI SABUNI AKIKABIDHI ZAWADI YA WALIMU WALIOWAFUNDISHA WANAFUNZI NYIMBO, NGONJERA, NA MAIGIZO KWA KATIBU TAWALA WILAYA MUHEZA BI DESDERIA HAULE | KATIBU TAWALA WILAYA YA MUHEZA BI DESDERIA HAULE AKIKABIDHI ZAWADI KWA WALIMU WALIOFUNDISHA WANAFUNZI NYIMBO, NGONJERA, NA MAIGIZO | KAIMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA NA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO AMBAYE NI DIWANI KATA YA ZIRAI SALIMU SECHAMBO AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAADHIMISHO. | AFISA MAENDELEO YA JAMII WILAYA YA MUHEZA BI. VIJE MFAUME NDWANGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA HAFLA HIYO. | WADAU WA WA TAASISI MBALIMBALI WAKIZUNGUMZA KATIKA HAFLA HIYO. NMB, WORLD VISION, CRDB NA ZICOSAD | WATAALAM WA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII WAKIWASILISHA MADA YA LISHE, MADAWA YA KULEVYA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO SIKU YA MTOTO WA AFRIKA TAREHE 16/6/2021 KATIKA KIJIJI CHA KWEMHOSI KATA YA NKUMBA | WANAFUNZI WAKIWA KWENYE MAANDAMANO NA BURUDANI MBALIMBALI SIKU YA MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRIKA JUNI 16,2021. | SEHEMU YA WANAFUNZI WALIOSHIRIKI, SHULE YA MSINGI MATOMBO, NKUMBA, NKUMBA KISIWANI NA SEKONDARI NKUMBA. | SEHEMU YA WANANCHI WALIOSHIRIKI |
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.