Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu sera, bunge, kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mheshimiwa Stella Ikupa amewahimiza watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) alipotembelea wilayani Muheza kujihusisha katika kilimo, ufungaji na ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi pia amesema kupitia mifugo na kilimo watapata lishe itakayowawezesha kuwa na afya njema. Pia katibu tawala wa wilaya ya Muheza amewatia moyo WAVIU kuwa “kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi sio mwisho wa maisha na sio mwisho wa kufanya kazi”.
Kadhalika Mheshimiwa Stella Ikupa ameiomba halmashauri ya wilaya Muheza kutoa elimu ya maambukizi ya ukimwi katika sehemu ambazo elimu haijawafikia na sio kutoa elimu mijini ambapo elimu ya ukimwi wanaipata mara kwa mara. Pia amewaomba kina baba kujitokeza kupima ukimwi hii ni kutokana na wanaume kuwaachia kina mama jukumu la kupima ukimwi hali inayopelekea ongezeko la maambukizi.
Vilevile Mheshimiwa Stella Ikupa alipata nafasi ya kutembelea kata ya lusanga na kuzungumza na kamati ya ukimwi kata ya lusanga amewaomba viongozi wa dini kutenga mda kanisani na misikitini kuzungumzia swala zima la athari za maambukizi ya ukimwi katika jamii “hii ni kutokana wananchi wanawaamini sana viongozi wa dini nawaomba sana wewe kama kiongozi wa dini tenga mda wa kuwaelimisha waumini wako juu ya athari za ukimwi, pia kuwahimiza kupima afya ili kujua kama wako salama”.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.