Kutokana na kuwepo kwa muitikio mdogo wa Wazazi kuhusu Elimu, pia kushuka kwa ufaulu Wilayani Muheza 2019. Ambapo hali ya ufaulu 2019 ni 65.3% umeshuka kwa 8.7% ukilinganisha na ufaulu Mwaka 2018 ulikuwa ni 74% kwa Shule za Sekondari,Watendaji wa Vijiji wameombwa kuwaelimisha Wazazi umuhimu wa Elimu. Yamezungumzwa katika kikao cha Elimu kilichofanyika katika ukumbi wa CWT lengo ni kutatua changamoto za Elimu na kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi wa Muheza.
Katika kikao hicho cha Elimu, Mratibu wa Elimu kata ya Kwakifua Ndugu Buzuka ameomba Watendaji pamoja na Wenyeviti wa Vijiji kuwaelimisha Wazazi umuhimu wa Elimu “ili tuweze kuongeza ufaulu ni lazima kuwepo na mahusiano mazuri kati ya Mzazi na Mwalimu naomba wadau wa Elimu, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji mtuungunishe sisi Walimu na Wazazi ili tuweze kuelewana naomba kutengenezwe kwa sheria ndogondogo ambazo zitawabana Wazazi” Amesema Buzuka.
Ameyasema hayo baada ya Afisa Elimu Happiness Laizer kutoa changamoto zinazowakabili katika eneo la Elimu kama vile upungufu wa Maabara, Vyumba vya Madarasa na Nyumba za Walimu, Wazazi kuruhusu watoto kushiriki vigodoro, utoro wa rejareja, ukosefu wa chakula mashuleni na upungufu wa Walimu 509.
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Nassib Mmbanga amewaomba Maafisa Elimu kuwashirikisha wadhibiti ubora katika kuchagua Walimu Wakuu ili kuweza kupatikana Walimu bora watakao saidia Watoto kufaulu “nawaomba Walimu mpendane ili muweze kufanya kazi kwa pamoja” amesema Mkurugenzi Mtendaji.
Vilevile Mkuu wa Wilaya ya Muheza amewaomba Walimu kufanya Kazi kwa haki na kwa uadirifu “naomba sitahiki za Walimu zifanyiwe kazi kwani Walimu wanafanya Kazi katika Mazingira magumu wanahitaji kupewa haki zao” amesema Mhe; Mwanasha Tumbo.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Muheza Bi. Happiness Laizer akiwasilisha Taarifa ya Elimu katika kikao cha Elimu kilichofanyika katika Ukumbi wa CWT |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.