Watanzania wametakiwa kumuenzi aliyekuwa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuzingatia na kufuata falsafa yake ya “HAPA KAZI TU” kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuliletea Taifa hili Maendeleo.
Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli alifariki mnamo tarehe 17/3/2021 majira ya saa 12:00 jioni katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dares salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo aliyokuwa akiishi nayo kwa Muda wa Miaka 10 sasa.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana tarehe 19/3/2021 katika ofisi yake mpya iliyoko katika kijiji cha Tanganyika kata ya Lusanga karibu na eneo la mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya Muheza Mkuu wa Wilya hiyo Mhe, Mwanasha tumbo amesema hayati DKT John Pombe Magufuli alikuw ni Mchapakazi, jasiri, mtetezi wa wanyonge , shujaa na mpenda maendeleo hivyo waanzania hatuna budi kumuenzi kwa falsafa yake.
Aliendelea kuwa marehemu Magufuli alipenda sana kufanya kazi zenye kuwaletea maendeleo watanzania ndio maana aliweza kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo na alihakikisha inakwisha kw wakati ulopangwa, kama vile barabara ya Muheza- Amani, Mradi wa maji kilapura, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, hospitali ya wlaya ambayo ni miradi itakayofanya watu wa Muheza wasimsahau daima.
Aliongeza kuwa kiongozi huyu aliweza kung’oa visiki vyote vigumu vilivyoachwa na muasisi wa kwanza wa Taifa hili hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere vilivyowanyima haki na kusababisha umaskini kwa watanzania ambavyo ni Rushwa , na Madawa ya kulevya.
Kadhalika aliwataka wananchi wa taifa la Tanzania kufanya kazi iliyo halali ndio maana aliweza kupambana na mafisadi, majambazi, wafanyabiashara ya madawa ya kulevya na wapenda rushwa kwani msingi wa vitu hvi ni kukosa haki.
Katika hatua nyingine aliwataka Watanzania kudumisha amani mshikamano , utulivu , upendo kwani ni miongoni mwa tunu za Tafa la Tanzania .
“Ndugu zangu Watanzania wenzangu tuwe watulivu, tudumishe amani, mshikamano, ili tuweze kuijenga Tanzania yenye upendo na utulivu” alisema Mkuu wa Wilaya Muheza.
Nao wafanya biashara wadogo wadogo waendesha pikipiki maarufu kama boda boda na wauza samaki wa wilayani Muheza wamesema wamesikitishwa kupotelewa na jemadali Magufuli kwa kuwa aliwasaidia kupata mikopo na kuwatengenezea barabara Muheza- Amani itakayowasidia kufanya biashara zao kirahisi.
|
|
|
|
Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe. Mwanasha Tumbo akizungumza namna alivyokipokea kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia Mheshimwa John Pombe Magufuli akiwa ofisini kwake Lusanga. | |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Viongozi wa Dini wakiomwombe Hayati Dkt John Pombe Magufuli na Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye anachukua nafasi ya Marehemu Magufuli mara baada ya kifo chake | Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza wakisaini kitabu cha Maombolezo kilichopo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Muheza jana tarehe 19/3/2021. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.