Watanzania wametakiwa kujiepusha na vitendo viovu vitakayopelekea kuvuruga Amani ya Nchi iliyoachwa na Mhasisi wa Taifa la Tanzania ambaye ni Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayyati Mwl Julius Kambarage Nyerere.
Ameyasema hayo Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Tumbo ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika Kongamano la Ibada Maalum ya kuombea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na kumuenzi Mhasisi wa Taifa ambaye kwa sasa amutimiza miaka 21 tangu alipoiaga dunia, ulliofanyika leo tarehe 14/10/2020 katika Uwanja wa jitegemee
Pamoja na hilo amewataka wananchi wa Muheza na Taifa kwa ujumla kufuata maadili ya dini ambayo humtaka mtu kutokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa na sheria ya nchi ikiwa ni sambamba na kutojihusisha na vitendo vya uchochezi , vurugu ili kulinda amani ya Nchi yet na kutoweka matabaka.
Mhe, Mwanasha amesema kuwa kwa yoyote atakayevunja sheria atachukuliwa hatua kwasababu ni mtu ambaye anahitaku hatarisha Amani.
Mbali na hilo pia amewataka wananchi kutodanganyika na mtu yeyote anaetaka kuuziwa kitambulisho cha mpiga kura ni kosa la jinai kutenda kosa hili kwa yeyote atakaethubu kufanya kosa hili awe muuzaji au mnunuaji atachukuliwa hatua za kisheria .
Lakini pia amewataka wananchi kupiga kura kwa Amani katika vituo vyao walivyojiandikishia na baada ya hapo wanatakiwa kurudi nyumbani ili kujiepusha na uchochezi utakaoweza kuleta ugomvi.
“Mwananchi yeyote aliyejiandikisha kupiga kura hakikisha anafika katika kituo alichojiandikisha na kupiga kura maana ni haki ya kila mmoja wetu hata vitabu vya dini vimesema kupiga kura ni haki ya mtu na ni dhambi kutokupiga kura” alisema Mkuu wa Wilaya Muheza.
Kwa upande wa viongozi wa dini wa Madhehebu ya dini zote wamesema suala la Amani ni jambo la msingi katika maisha ya binadamu hivyo basi kila mmoja azingatie hilo na kwenda kinyume na mwenyezi mungu ni kumkosea na adhabu yake ni kubwa kwake.
Viongozi wa dini wa Madhehebu mbalimbali wakizungumza wakati wa ibada | Viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo iliofanyika katika uwanja wa jitegemee tarehe 14/10/2020 | Wajumbe wa kamati ya Amani ya Wilaya Muheza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ibada kukamilika |
Sehemu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza walioshiriki katika kongamano hilo. |
|
Mamia ya wananchi walioshiriki katika kongomano la ibada maalum ya kuombea uchaguzi ili ufanyike kwa njia ya amani iliofanyika katika uwanja wa jitegemee tarehe 14/10/2020 ikiwa ni siku ya kumbukizi ya miaka 21 ya kifo cha Mwl Nyerere. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.