Mratibu wa chama cha wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Tanga Bi Flora Urassa amesema watumishi wawaliomaliza muda wao wa kuitumikia serikali (wastaafu) hawatolipwa mafao ya mkupuo kama awali bali watalipwa asilimia 25 na asilimia 75 inayobaki watalipwa kama mshahara wa kila mwezi ili kuwasaidia wastaafu waendelee kuishi maisha mazuri kama walivyokuwa kazini.
Akizungumza na wafanyakazi, wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya ( TUGHE) Kilichofanyika jana katika ukumbi wa Mikutano wa ofisi za Mji Urassa alisema mabadiliko haya yameanza kufanyiwa kazi mnamo Tarehe 1/8/2018, hivyo basi watumishi waliostaafu baada ya tarehe hii watahesabiwa mafao yao kwa kutumia sheria hii.
“Serikali imeamua kuanzisha sheria Mpya ya Mafao na kuondoa baadhi ya mafao kama vile Fao la Uzazi baada ya kuona wafanyakazi wakisha staafu wengi wao huzitumia Pesa vibaya walizopata na hatimaye kuendelea kutegemea Serikali hali inayoipelekea Serikali kuwa na ongezeko kubwa la wategemezi” alisema Flora.
Aliongeza kuwa sheria hii itawanufaisha wastaafu kwani watakuwa na uwezo wa kukopesheka hivyo basi kuendelea kuishi Maisha bora yenye furaha daima wakati hapo awali walipewaasilimia 100 ya mafao ambapo baada ya hapobwalikuwa wakilipwa nusu mshahara hali iliyopelekea kuishi maisha yasiyoridhisha.
|
|
|||||||||
|
|
|||||||||
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.