Mapema leo msimamizi wa uchaguzi Pascal John Temba ametoa elimu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa kuhusu majukumu yao katika kusimamia, kuendesha na kushiriki uchaguzi. Pia kufahamu haki na wajibu wa wapiga kura na vyama vya siasa, kadhalika amewaambia" mgombea au mtu aliyeomba kuteuliwa anaweza kuweka pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea na sio mpiga kura".
Vilevile Rehema Akida msimamizi msaidizi wa uchaguzi amewaomba wasimamizi wasaidizi kusoma miongozo vizuri ili waweze kutoa maelekezo sahihi kwa viongozi wa vituo, pia amewaomba kuhakikisha wanashirikisha vyama vya siasa bila kujali itikadi.
Pia semina iliambatana na zoezi zima la kiapo ambapo wasimamizi wasaidizi waliapa kwaajili ya kuanza kufanya kazi ya uchaguzi. Alimalizia kwa kuwaomba wasimamizi wasaidizi kufanya uchaguzi wa haki pia kuhakikisha wanaimarisha demokrasia pia amemalizia kwa kuwaomba kufanya kazi kwa weredi.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.