Wanawake Wilaya ya Muheza wamejitolea kuchimba Msingi wa chumba cha Darasa katika Shule ya Msingi Muheza Estate iliyopo kata ya Tanganyika leo tarehe 07/03/2020 lengo ikiwa ni kutatua changamoto ya upungufu wa Madarasa katika Shule hiyo kama sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Akizungumza Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Bi Vije Ndwanga amesema “sisi kama Wanawake tumeona tujitolee kuchimba Msingi wa Darasa moja, kama sehemu ya kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto ya upungufu wa madarasa pia kuwahamasisha wadau wa Elimu kuona ipo haja ya kujitolea katika swala la Elimu kumekuwa na changamoto ya upungufu wa Madarasa katika Shule hii hali inayopelekea Wanafunzi kusoma katika Mazingira Magumu hata kusababisha kushuka kwa ufaulu kwa Wanafunzi”.
Sambamba na hayo Bank ya NMB waliweza kukabidhi mifuko Miwili ya Cement kwa Afisa Mtendaji Bwana Hashimu kwaajili ya zoezi zima la ujenzi wa Darasa katika Shule hiyo kama sehemu ya kuunga Mkono juhudi za Wanawake wa Muheza katika kutatua changamoto za Elimu Muheza.
Afisa Mtendaji Kata ya Tanganyika akipokea mifuko ya Cement Miwili kutoka Bank ya NMB | Moja ya kina Mama wa Muheza akiwa anachimba Msingi wa chumba cha Darasa Shule ya Msingi Mkurumuzi iliyopo kata ya Tanganyika
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.