Tarehe 3/2/2025 Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Muheza Mheshimiwa Lusajo Mueni Mutua ameongoza maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini katika viunga vya Mahakama ya Wilaya ya Muheza iliyopo kata ya Mbaramo. Maadhimisho haya yalitanguliwa na Wiki ya sheria iliyoanza tarehe 25/1/2025 mpaka leo yakiwa na lengo lakuwakumbusha wadau na wananchi umuhimu wa utawala wa sheria.
Aidha mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Muheza ambae pia ni Afisa Tarafa ndugu Ally Kijazi amewataka Wananchi wasikae kimya pale ambapo mambo yasiyokua mazuri yakiendelea katika maeneo yao wanayoishi kama mambo ya unyanyasaji na ulawiti pia watoe ushirikiano wa kutoa ushahidi mbele ya Mahakama.
“Mwenye Haki apewe haki asie na haki aelezwe ukweli na utaratibu wa kisheria kwamba jambo hili halipo sawa kwahiyo mwenye haki asicheleweshewe haki yake”.
Nae Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Bi Anjela Mwapachu ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza inapokea Wananchi mbalimbali kupitia kitengo cha Sheria na kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi, talaka na malezi ya Watoto na kutoa ushauri mbalimbali utakaosaidia kutoa suluhu au kuwaongoza Mahakamani kupatiwa haki.
Katika hotuba yake Mheshimiwa Mutua amesema kuwa hadi sasa Mahakama imefanikiwa kusikiliza kesi za Madai na Jinai Mashauri 161 yaliyobaki hadi sasa ni 27 huku Mahakama za Mwanzo Mashauri 910 yamesikilizwa na yaliyobaki ni 64 tu.Takwimu hizi zinajumuisha Mahakama zote za mwanzo ndani ya Wilaya ya Muheza kwa mwaka 2024/2025.
Siku hii iliyoambatana na Kauli mbiu ya “TANZANIA YA 2050: NAFASI YA TAASISI ZINAZOSIMAMIA HAKI MADAI KATIKA KUFIKIA MALENGO MAKUU YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO”, Mheshimiwa Mutua amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa jamii na amewasisitiza wananchi na wadau wote kuwa wanahaki ya kupata huduma za kisheria hivyo wawe mstari wa mbele kupata haki zao.
“Na wale walio karibu na viunga vya mahakama muda wowote saa yoyote wafike ofisi zipo wazi tupo kwa ajili ya kuwahudumia
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.