Afisa Elimu Msingi wilaya Muheza Bi Pili Maximillan amesema wanafunzi wa darsa la nne wataanza Mitihani ya Taifa ya siku mbili kuanzia kesho Tarehe 22/11/2018 na kumaliza Tarehe 23/11/ ambapo Mtihani wa upimaji wanafunzi wa ufundi utakuwa wa siku 3 kuanzia Tarehe 21/11/2018 hadi tarehe 23/11/2018.
Akitoa taarifa ya wanafunzi Wa darasa la nne watakaofanya Mtihani wa Taifa 2018 jana katika Semina ya Wasimamizi wa mitihani iliyofanyika ukumbi wa Taleku Maximillan alisema jumla ya watahiniwa ni 5918 kati yao wavulana 3038 na wasichana 2880 watafanya mtihani katika shule zote za msingi 116 kati ya hizo 111 ni za serikali na 5 ni za watu binafsi na mashirika ya dini.
Aidha, kwa upande wa wanafunzi wa ufundi stadi watahiniwa 46 watafanya mtihani kati yao wavulana 22,na wasichana 24 ambao watafanya mtihani katika kituo kimoja cha Shule ya Msingi Magila.
Nae Afisa Elimu Taaluma Sekondari Bwana Richard Msagati alitoa taratibu kwa wasimamizi wa Mitihani kuwa kabla ya kuanza mtihani wahakikishe wanafunzi wanakwenda kujisaidia kwani hawaruhusiwi kutoka nje kabla mtihani kwisha, wasibadilishe mpangilio wa madawati, wasimhamishe mtahiniwa kutoka kwenye nafasi yake, wasisimame sehemu moja, wawe wanazunguka darasa zima ili wasiwatie hofu watahiniwa na wale wasiojua kusoma KKK wajaziwe fomu na M-1.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.