Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mheshimiwa Mwanasha Tumbo ameshiriki chakula cha pamoja na watoto 420 wanaoishi katika mazingira magumu, walemavu na yatima kutoka Afrihovic na wanafunzi wanaosoma shule za Mbaramo, Masuguru na Mlingani WIlayani Muheza Jana Agosti 22, 2018 katika Ukumbi wa Tareku.
Pamoja na kushiriki nao chakula katika sikukuu hiyo Mheshimiwa Tumbo aliwahi kuwapatia watoto hao baadhi ya mahitaji yao ya shule kama vile madaftari, kalamu. Pia aliwafungulia akaunti ya benki jumla ya watoto 296 na kuwapatia bima ya afya ili waweze kupatiwa matibabu bure pindi wanapopatwa na maradhi, alifanya hivyo ili kuwawezesha watoto hao kuendelea kufaulu vizuri katika masomo yao kwasababu wazazi wao hawana uwezo wa kukidhi mahitaji yao.
Aidha aliwahamasisha wadau walioshiriki katika hafla hiyo kuanzisha mfuko wa kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi Muheza na hatimaye kiasi cha Tsh 330,000/= kilipokelewa na ahadi ya Tsh. 1,805,00/= , vile vile alitoa zawadi kwa watoto waliofaulu vizuri kuanzia mwaka 2017 kwenda 2018 kwa ajili ya kuwahamasisha wanafunzi wengine waongeze jitihada katika masomo yao.
Pia alipata fursa ya kutembelea kituo cha kulelea Wakoma katika Kitongoji cha Misufini kijiji cha Umba Kata ya Ngomeni ambapo jumla ya walemavu 25 walipatiwa kondoo mmoja, mafuta kupikia ndoo moja na mchele kilo 50 ili waweze kusherehekea sikukuu hiyo kwa furaha.
Kwa upande mwingine alikabidhiwa Ng’ombe 88 na kondoo 100 katika kata ya Mkuzi na asasi ya kiislam ijulikanayo kwa jina la Islamic Help kwa ajili ya kuchinja siku ya Eid, Pia aliwasihi wananchi waendelee kuwa na uvumilivu kwani watagaiwa kitoweo hicho kikishachinjwa.
Nae Mheshimiwa Diwani wa kata ya mkuzi Bi Sharifa Kivugo ameendelea kuwasisitiza wananchi waendeleekuwa wavumilivu kwani kitoweo hicho kitagaiwa kwa kila kitongoji.
Chakula cha pamoja na watoto 420 wanaoishi katika mazingira magumu |
||
|
|
|
Mhe. Tumbo(Aliekatikati) akishauriana jambo na Wanakamati wa maandalizi wa sherehe hizo
|
|
Madiwani na Wanafunzi wakiwa katika hafla hiyo |
|
|
|
|
|
|
Mhe. Tumbo. wanakamati na Wadau mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja. |
|
Mhe. Tumbo akimkabidhi zawadi mwanafunzi aliefanya vizuri darasani
|
|
Mwanafunzi mwenye ulemavu vya viungo shule ya Msingi Kwafungo, Maimuna akikata keki kwa mdomo siku ya Eid El Haji |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.