Wajumbe wa Kamati ya siasa wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga imetoa pongezi kwa viongozi wa Serikali na Chama wa Wilaya ya Muheza kwa namna walivyoweza kutekeleza Ujenzi wa Miradi ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa dhidi ya Mapambano ya Uviko-19.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi( UVCCM) Mkoa wa Tanga Rasul Shandala ambae alikuwa kiongozi kwenye ziara ya kukagua Ujenzi wa Miradi.
“Alimesema viongozi hao wamemsaidia Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe, Samia Suluhu Hassan kazi kumbwa ambayo inakwenda kuonyesha dhamira ya Maendeleo kwa Watanzania kwafedha hizi zimeweza kusaidia Wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kama ilivyo kuwa dhamira yake” Rasul
Awali Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Muheza Like Gugu amewaomba Wanachama na Watanzania kuendelea kuunga Mkono juhudi ambazo zinafanywa na Mhe, Rais Samia Suluhu Hassani za kuendelea kupandisha uchumi wa Taifa.
“Alisema Mhe, Rais amefikilia kwa umakini na kuamua fedha hizi ziende kujenga Shule na katika shughuli hizo za ujenzi vifaa vyote vitoke kwenye viwanda vyilivyopo Tanzania na Mafundi watumike vijana wa Tanzania kwenye maeneo hayo jambo ambalo limechangia kukuza uchumi miongoni mwa Watanzania” Gugu.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo ambae ndio Kamisaa wa Chama Wilaya amesema Mafanikio ambayo yameonekana leo ni kutokana na ushirikiano uliokuwepo Miongoni mwao viongozi wa Chama na Serikali wakiwemo Madiwani pamoja na Wananchi katika kushiriki kwenye Miradi hiyo.
“Alisema kuwa Wananchi wa Wilaya ya Muheza wanamshukuru Mhe, Rais wa Tanzania kwa kitendo cha kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 67 hivyo ameongeza kwa kusema kuwa ana muhakikishia Mwenyekiti wa Chama Taifa na Rais wa Tanzania kuwa watamshukuru kwa vitendo na sio Maneno katika kusimamia Miradi mbalimbali ambayo Wananchi wa Muheza wataendelea kupatiwa” DC Bulembo.
|
|
|
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi( UVCCM) Mkoa wa Tanga Rasul Shandala (katikati) akisisitija jambo kwa viongozi wa chama na Serikali mara baada ya kukagua vyumba vya madarasa
|
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza Dkt, Flora Kessy akisoma taarifa ya Ujenzi wa kituo cha Afya kwafungo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya siasa wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga na viongozi wa wilaya ya Muheza.
|
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Halima Bulembo (kushoto) akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya siasa wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga katika ukagunzi wa Bweni la Watoto wenye Mahitaji Maalumu katika shule ya Msingi Ngomeni.
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.