Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe,Mhandisi Mwanasha Rajabu T umbo atoa agizo la kusitisha muziki wa sherehe za usiku za majumbani ujulikanao kama( kigodoro) baada ya tabia za uvunjifu wa maadili kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kukithiri shuleni, aliyasema hayo jana katika kikao cha wadau wa elimu wilayani humo.
Akizungumza na wadau wa elimu ndugu Mwanasha alisema kuwa vigodoro visiruhusiwe kwani ndio chanzo cha ongezeko la utoro shuleni hivyo basi kupelekea wanafunzi kutofaulu vizuri darasani na aliendelea kumsisitiza Afisa utamaduni Wilaya asimamie sheria ya utoaji vibali vya muziki
Kwa upande mwingine aliitaka jamii kusimamia ipasavyo ulinzi na usalama wa mtoto hatimaye kutokomeza ukatili ukatili unaofanyika dhidi ya watoto.
“jukumu la kumlea mtoto ni jukumu la kila mmoja wetu katika jamii hivyo basi kila mmoja kwa nafasi yake asimame imara kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto unatelekelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na pamoja na kuhakikisha ukatili dhidi ya mtoto unatokomezwa” alisema mwanasha tumbo
Akitoa ufafanuzi wa utaratibu na kanuni za vigodoro, Afisa utamaduni Wilaya Muheza ndugu Msafiri Nyaluva amesema kigodoro ni muziki wa sherehe za usiku zifanyikazo nyumbani ambao huanza saa 10:00 jioni mpaka saa 6:00usiku, watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kujihusisha na sherehe hizo kwani mara nyingi ndani ya muziki hii kuna vitendo viovu vinavyofanika ambavyo hupelekea kuvunjika kwa maadili.
Akiunga mkono kauli ya mkuu wa wilaya Nyaluva amesema atahakikisha muziki unazimwa mapema kama kanuni na taratibu zinavyota kwanivigodoro husababisha kuenea kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwani kuna vitendomara nyingi wamekuwa wakijihusisha na mapenzi , vigodoro vimekuwa chanzo cha kelele kwa jamii, taassisi za dini misikiti na kanisa na nyumba za kulala wageni.
Pia ameitaka jamii kufuata kanuni na taratibu za sheria za kibali zilizopo, wenye sherehe wahakikishe wanazima muziki ndani ya muda uliopangwaharaka iwezekanavyo, watoto wasiende wasiruhusiwe kwenda kwenye vigodoro na alisisitiza kuwa yeyote atakaekwenda kinyume na taratibu atachukuliwa hatua za kisheria.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.