Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan awezesha upatikanaji wa Bilioni 1.7 Katika uzinduzi wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyofanyika kwenye ukumbi wa Golden Tulip(Masaki) jijini Dar es Salaam Jana Machi 16, 2018.
Akizungumza na wadau walioalikwa Katika harambee Hiyo, Samia amesisitiza na kutoa wito kwa wadau na wananchi kwa ujumla Katika kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi na uboreshwaji wa Huduma za kijamii Kama Huduma ya Afya.
"Niwakumbushe kuwa mjenga nchi ni mwananchi, na hivyo ujenzi huu ni hatua kubwa inayofaa kuungwa mkono na serikali, lakini pia wadau wote wa maendeleo na wanaoitakia mema Tanzania." Alisema Samia.
Aidha Samia alizitaka TAMISEMI na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto zione namna gani zinaweza kuratibu upatikanaji wa vifaa na watumishi wa hospitali hiyo pindi ujenzi utakapokamilika.
Pia Makamu wa Rais aliwapongeza uongozi wa Mkoa wa Tanga na Wilaya ya muheza kwa kuona changamoto na kutoa kipaombele katika upatikanaji wa huduma ya Afya Wilayani hapo, na kwa kuzingatia kuwa afya bora ni moja ya kigezo kinachochochea kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nguvu kazi ya taifa, na hivyo kupelekea Tanzania kufikia malengo yake ya kuwa na uchumi wa kati.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema, katika kufanikisha ujenzi huo kila mwana Muheza ameahidi kutoa Tsh. 2000 na nguvu kazi kama mchango wao katika ujenzi wa Hospitali hiyo.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella na Mbunge wa Jimbo la Muheza,Mhe. Adadi Rajab.
JINSI YA KUCHANGIA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA KWA KUTUMIA MITANDAO YA SIMU.
M-PESA nenda menu *150*00#
TIGO PESA nenda menu *150*01#
Kwa mitandao ya ;
AIRTEL,ZANTEL,TTCL&HALOTEL namba ya kampuni ni 395544
Mfumo uliowezeshwa bure na kampuni ya Maxcom Africa PLC(MaxMalipo)
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.