Mwakilishi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza ambaye ni Msimamizi Msaidizi ngazi ya Jimbo na Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Aisha Mhando amefungua mafunzo ya siku 2 kuanzia tarehe 23/10/2020 hadi 24/10/2020 kwa wasimamizi wasaidizi 555 wa vituo 164 vya Tarafa ya Muheza yenye kata 14 na kata ya Kwezitu.
Akizungumza katika Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Tate plus uliopo katika kata ya Genge Bi. Aisha amewataka wasimamizi wasaidizi wa vituo hivyo wafanye kazi hiyo kwa uadilifu na utekelezaji wa yale yote watakayoelekezwa katika semina hiyo ili kuleta ufanisi mkubwa katika kazi hiyo.
Aidha amewasisitiza kutoonyesha Ushabiki wa Vyama vya siasa ili kuepukana na mgogoro unaoweza kujitokeza wakati wa zoezi la upigaji kura litakapoanza.
Sambamba na hayo, aliwaongoza wasimamizi wasaidizi hao kula kiapo cha kutunza siri kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO WAKIAPISHWA | WAWEZESHAJI AMBAO NI WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA WAKITOA MAFUNZO. |
|
|
||
|
|
|