Mkurugenzi wa Taasisi ya Human bridge yenye makao makuu SWEEDEN Bwana Bahati Titto akabidhi akabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya TZS Milioni 400 kwa viongozi wa Wilaya Muheza leo katika jengo la kuhifadhia dawa ili visambazwe katika vituo vyote vya kutolea huduma.
Aidha amewataka viongozi wa wilaya kuvisimamia kwa karibu vifaa tiba hivyo kwa kuhakikisa vinahifadhiwa mahali salama na kufanyiwa marekebisho ma matengengezo mara kwa mara , pia aliwataka wavitumie vifaa hivyo wakati wote vinavyohitajika badala ya kuviihfadhi ndani bila ya kuvifanyia kazi . amesema kwa wataalam wasioweza kutumia teknolojia hiyo waelimishwe kwani ni vifaa vya kisasa.
Akisoma taarifa ya vifaa vilivyokabidhiwa Mganga Mkuu wa Wilaya Bi Flora kessy amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni vitanda, ultrasound, magodoro, wheel chairs, vifaa vya upasuaji, vifaa vya macho, vifaa vya masikio , mashine ya usingizi , mashine ya upumuaji, sare za wauguzi , wagonjwa na madaftari ya watoto wenye mahitaji maalum ambapo ameahidi kuvitunza na kuvisambaza katika vituo vya kutolea huduma .
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya bw Nassib B. Mbagga amesema atavitunza na kuvigawa kabla ya siku 14 na ametoa shukrani za dhati kwa Taasisi hiyo kwa kuweza kutambua kilio cha wana muheza .
Kwa upande wa Mbunge wa jimbo la Muheza Mhe, Adadi Rajabu ameishukuru Taasisi ya human bridge kwa kusikia kilio chake kwani ni jambo alilokuwa akilifuatilia sana alipokuwa bungeni pia alimuagiza Mganga mkuu kuvisimamia kwa karibu vifaa hivyo na kuhakikisha vinagawanywa katika vituo vyote vya kutolea huduma.
Mkurugenzi wa human bridge akikabidhi vifaa tiba kwa Mkuu wa Wilaya.
|
|
viongozi wa wilaya Muheza wakikagua vifaa tiba
|
---|---|---|
|
||
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.