Serikali inatekeleza mpango wa Anwani za Makazi ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Posta ya Mwaka 2003, Makubaliano ya kimataifa (PanAfricanPostal Union (PAPU), Univesal Postal Union (UPU) na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2020- 2025 kifungu Na. 61(m) zinazoelekeza kuhakikisha Anwani za Makazi zinawekwa nchini ili kurahisisha upatikanaji, utoaji na ufikishaji wa huduma katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza katika kikao cha Viongozi wa Mamlaka ya Mji wa Muheza kilichohudhuriwa na wenyeviti wa vitongoji na wataalam wa Mji huo Mratibu wa Anwani za Makazi ambaye pia ni Afisa Tehama wilaya ya Muheza Mkumbo Levi Ngoi amesema Anwani ya Makazi ni utambulisho wa Mahali mtu/kitu kilipo juu ya uso wa Nchi.
Aliendelea kufafanua kuwa Anwani ya Makazi inaundwa na vitu vitatu (3) ambavyo ni namba ya nyumba/ jengo, Jina la barabara/Mtaa na Postikodi ambavyo husaidia kutambulisha mahali husika.
Akizitaja faida za Anwani za Makazi Mkumbo amesema zina tija kiuchumi na kijamii ambazo huchangia kuimarisha ulinzi na usalama, hutengeneza ajira, husaidia kufanya biashara mtandao, husaidia kufanya tafiti lakini pia hupunguza gharama za upatikanaji wa huduma.
Awali akielezea Muda wa ukamilishaji wa zoezi la Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza THOMAS MKWAVI amesema zoezi la Anwani za Makazi linatakiwa kukamilika mnamo mwezi MEI 22, 2022 hivyo basi viongozi waharakishe zoezi la kubaini Majina ya Barabara na Mitaa.
“zoezi hili ni Muhimu sana kwa maisha ya sasa na ya baadaye hivyo basi tufanye kazi kwa moyo kwa ajili ya Vizazi vijavyo” alisema Mkwavi.
MRATIBU AKITOA MAELEKEZO | AFISA MIPANGO MIJI (W) MUHEZA AKIELEKEZA | AFISA MIPANGO MIJI MSAIDIZI AKIELEKEZA |
Mratibu wa Anwani za Makazi akitoa MKUMBO LEVI NGOI akitoa maelekezo kwa wajumbe | Afisa mipango Miji (w) Muheza THOMAS MKWAVI akielezea jambo | Afisa mipango miji msaidizi HAPPINESS NAMPONJI akifafanua jambo |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.