Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omari Mgumba amewataka Waheshimiwa Madiwani na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kushirikiana kwa pamoja katika shughuli mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo Wilayani humo.
Ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika siku ya jumatatu tarehe 5/9/2022 alipokwenda kujitambulisha kwa mara ya kwanza baada ya kuhamishiwa katika mkoa wa Tanga.
Amesema maendeleo ya wananchi wa Muheza yatapatikana na kuboreshwa kama waheshimiwa madiwani na kamati ya wataalam wa Halmashauri hiyo (CMT) watafanya kazi kama timu na kuwa kitu kimoja katika mipango wa utoaji wa maamuzi ya masuala mbali mbali ya maendeleo ya Wilaya ya Muheza hususani mipango ya utekelezaji miradi ya maendeleo.
“Nyinyi ndio mliopewa mliopewa jukumu la kusimamia Serikali ya Halmashauri ya hapa Muheza, nyinyi ndio mnaopanga mapato na matumizi kupitia kamati yenu ya fedha kila mwezi na nyinyi ndio mnaosimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua miradi kila mwezi au kila baada ya miezi mitatu kama kuna miradi mibovu, matumizi mabovu baraza la madiwa linahusika kwa kuwa majukumu ya usimamizi wa miradi hiyo mmepewa kisheria na kikatiba” alisema Mgumba.
Aliendelea kuwa mkifanya kazi kama timu mtapunguza na kuondoa malalamiko, mivutano na makundi yanayoweza kupelekea kuchelewesha ukamilishaji wa miradi ya maendeleo iliyopangiwa fedha na Serikali hivyo basi kushindwa kufikia adhima ya Seikali ya kuwapatia wananchi wake maendeleo.
“Sitomvumilia mtu yeyote mwenye nia ovu ya kumchonganisha Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na wananchi kwa kushindwa kutekeleza wajibu na majukumu yake kwa kuwacheleweshea wananchi maendeleo” aisisitiza Mhe. Mkuu wa Mkoa.
Kwa upande wake kaimu Mkuu wa Wilaya ya Muheza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Shaibu Lingo amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kupitia ofisi yake yaandaliwe mafunzo kwa waheshimiwa madiwani yatakayolenga kuwakumbusha wajibu na majukumu yao ili waweze kuzingatia taratibu, kanuni, miongozo na sheria za nchi na atakaeshindwa kuzingatia maelekezo hayo hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Nae kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ambaye pia ni Afisa Mifugo na Uvuvi wa Wilaya hiyo Edward Mgaya amesema kwa niaba ya wafanyakazi wa Muheza wapo tayari kushirikiana na kufanya kazi kama timu na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri hiyo.
KAIMU MKUU WA WILAYA YA MUHEZA AKIZUNGUMZA | MWENYEKITI WA HALMASHAURI AKIZUNGUMZA WAKATI WA KIKAO | SEHEMU YA MADIWANI NA WAKUU WA IDARA |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.