Taasisi ya kifedha ya NMB tawi la Muheza pamoja na taasisi ya ‘DiraA Women Organization’ (DIWO) yenye makao Makuu Dar es salaam wametoa jumla ya T-shirt 24 zenye thamani ya shilingi laki tatu na elfu arobaini na mbili (342,000) kwa watu wenye ualbino 11 na kiongozi wao, wakiwemo wanafunzi 6 wa Shule ya Sekondari MLINGANO.
Wakizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Taasisi ya kifedha ya NMB Meneja wa Nmb tawi la Muheza Ndugu Anna Chimalilo na Mkurugezi wa taasisi wa DIWO wamesema lengo la kuwapatia T-shirt hizo ni kuwasaidia kwenda kwenye kongamano la kimataifa la maonyesho ya kazi zinazofanywa na watu wenye ualbino linalotarajiwa kufanyika tarehe 10/6/2022 hadi 13/6/2022 Mkani Kagera.
Katika tukio linguine Meneja wa Benki a NMB tawi la Muheza amemkabidhi Afisa elimu Maalum Wilaya ya Muheza Ndugu Muumin Sudi Wabu fedha taslimu kiasi cha shingi laki moja na elfu thelathini (130,000) kwa ajili ya kujikimu wakiwa safarini humo.
Kwa upande wake Afisa Elimu Maalum wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza MUUMIN SUDI WABU amewashukuru viongozi wa Muheza wakiwemo Mbunge wa jimbo la Muheza Hamisi Mwinjuma, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Nassib Mmbagga, taasisi ya kifedha NMB na DIWO kwa kufanikisha safari ya wanafunzi hao.
Nao watu wenye ualbino wametoa shukrani kwa viongozi na wadau wote kwa michango waliyoitoa na kuahidi kuiwakilisha vyema Muheza katika maonyesho hayo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.