Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulege amefunga kambi ya Vijana CCM Mkoa waTanga leo baada ya kumaliza muda wao wa ushiriki wa siku 14 katika Ujenzi wa Hospitali ya wilaya muheza ambao ulianza tarehe 10/09/2018 hadi 25/9/2018.
Akisoma taarifa ya kufunga kambi ya umoja wa vijana CCM Mkoa wa Tanga, Katibu wa CCM Mkoa Tanga Ndugu Zawadi Hussein Nyambo amesema lengo la kambi hiyo ni kujenga Hospitali ya wilaya ambapo wameweza kushindilia kifusi, kupanga mawe,na kumwaga zege la jamvi ,pia kusoma masomo mbalimbali ya ujasiriamali, ukakamavu na uzalendo kwa vijana, hali itakayopelekea vijana kutojihusisha na Madawa ya kulevya na UKIMWI.
Akiendelea kusoma taarifa hiyo Zawadi amesema kutokana na usikivu na uelewa wa Vijana walioshiriki hapa kambini wapatao 300, ambapo ME 232 na KE 68, tuna imani kwamba watakuwa walimu na wajasiriamali waliokamilika kwani wameanzisha Kikundi cha Vijana kiitwacho OMARI MWANGA REVOLUTION GROUP kitakachokuwa kinatoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya zote za Mkoa Tanga ili kuwajengea uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza sabuni, ya maji, mishumaa, keki, chaki,na batiki. Pia aliitaka serikali kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.
Kwa upande mwingine Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Ndugu Mathias Abuya amesoma taarifa ya ujenzi kuwa utekelezaji wa ujenzi huo utagharimu kiasi cha Tshs 11,322,459,300 (bilioni kumi na moja milioni mia tatu ishirini na mbili mia nne hamsini na tisa elfu na mia tatu) ambayo inajumuisha ujenzi wa majengo na vifaa.
Akiendelea kusoma taarifa hiyo Abuya alisema Halmashauri ya Wilaya imetenga kiasi chaTshs 150,000,000/ kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali kuu imetenga kiasi cha Tshs 1,500,000,000/kwa Mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya kuendeleza mradi pia vijana wa CCM Mkoa Tanga wameokoa kiasi cha TSHS 11,000,000.
Nae mkuu wa Wilaya Muheza Mhe Mwanasha Rajabu Tumbo amemshukuru Naibu waziri na wadau wote waliofika pale, pia alitoa kiasi cha tshs 500,000kwa vijana ili kuwatia nguvu ya kutumikia Kutumikia Taifa la Tanzania na kuwasihi kuendeleza umoja na mshikamano kwani yuko tayari kushirikiana na wilaya nyongine kwa lolote.
Akitatua changamoto ya Ajira kwa Vijana Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulege liwaagiza wataalam mbalimbali wa mifugo kuunda vikundi vya VijanaVya Ujasiriamali, visajiliwe kisha wakopeshwe ng’ombe wa Maziwa kwa ajili ya kupata Maziwa na kupeleka Kiwandaniili wajikwamue kiuchumi. Pia ameahidi kuwaletea kuku na wataalam watakao waelimisha Vijana katika ujasiriamali wa kutengeneza sabuni na zao la Mwani ambalo hulimwa kwenye Pwani ya Bahari. Alitoa agizo la siku 14 kwa Mwenyeiti wa vijana CCM Mkoa Tanga na wataalam wa Mifugo na Uvuvi kuhakikisha vijana wanapata fursa za kujikwamua kiuchumi. Pia alitoa kiasi cha Tshs 1,000,000 kwa vijana kwa ajili ya kuwahamasisha kuendeleza ujenzi huo.
|
|
|
|
Mkuu wa wilaya muheza Mhe, Mwanasha Rajabu Tumbo mwenye nguo nyeusi akijadiliana jambo na Katibu CCM wilaya Muheza Ndugu Mohammed Moyo | Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe, Abdallah Ulege mwenye shati la bluu akiwa kwenye picha ya pamoja na vijana wa CCM Mkoa Tanga. |
---|---|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.