Naibu Waziri wa Madini Ndugu Dotto Mashaka Biteko afanya ukaguzi wa eneo lililofunguwa leseni ya uchimbaji wa madini kwani lipo kwenye kwenye chanzo cha maji katika kitongoji cha kwasempasi kijiji cha sakale kata ya mbomole jana Tarehe 13 Agosti 2018.
Ndugu Dotto alianza kuwakaribisha wananchi watoe michango yao na waeleze hali halisi ya uchimbaji wa madini Sakale.
Mkazi mmoja wa kitongoji cha Ngoka Bw. Amari Abdallah Tindi alianza kutoa shukrani kwa Mbunge Adadi Rajabu kwa kumleta Naibu Waziri wa madini na kusema kwamba anaomba mgodi ufunguliwe kwani eneo hilo lina madini mengi ambayo yakichimbwa yataweza kubadilisha maisha yao kiuchumi.
Pia aliahidi kuwa iwapo mgodi utafunguliwa watafuata taratibu zote za Serikal kama za ulipaji kodi na uhifadhi wa mazingira na misitu,nae Mwenyekiti wa kijiji cha Sakale Ndugu Abdallah Mahafudhi amesema mnamo mwaka 2003 walipewa leseni wakaanza kuchimba bila kuharibu mazingira na misitu lakini baada ya watu wengi kuingia ndio uharibifu ukaanza hivyo basi wanaomba wapewe leseni kwani watafuata taraibu zote za uhifadi wa mazingira.
Nae mmiliki wa eneo la uchimbaji Ndugu Abdi Selemani alimuomba Naibu Waziri atoe ruhusa kwa wananchi wachimbe madini kwani vijana wengi hawana kazi ambapo imepelekea kuwa waporaji wa mali za watu majumbani, aliongeza kuwa, elimu itolewe kwa wachimbaji juu ya uhifadhi wa vyanzo vya maji, misitu, na mazingira.
Pia Mbunge wa jimbo la Muheza ndugu Adadi Rajabu alimuomba Naibu Waziri atume timu ya wataalam waje wapime ili kujua mgodi uliopo ni mkubwa kiasi gani na kama uko kwenye chanzo cha maji na uhifadhi wa mazingira na kama haupo kwenye hifadhi yoyote basi wananchi wachimbe kwani wameweza kutunza mazingira.
Aidha ndugu Mashaka Biteko amewashukuru wananchi wa Sakale kwa uvumilivu kwani walipofungiwa kuchimba madini walivumilia hawakuleta vurugu pia amewataka waendelee kuvumilia kwani atatuma timu ya wataalam wapime eneo hilo ili ikionekana kuwa halitaleta athari za kimazingira watapewa ruhusa ya kuchimba madini kwaajili ya kuleta maendeleo ya kiuchumi katika familia zao.
“ Naomba niwashukuru wana Sakale kwa utulivu wenu kwani baada ya kufungiwa kuchimba madini mliweza kutulia Pia kuweni na subira msilete vurugu kama mnataka kujaribu endeleeni kujaribu, usione vyaelea ujue vimeundwa” alisema naibu waziri.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.