Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na watoto atembelea Muheza katika taasisi ya awali ya utafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR) iliyopo katika kata ya Amani ambayo kwasasa inatarajiwa kuwa chuo cha utafiti wa tiba na magonjwa ya binadamu baada ya taasisi hiyo kuhamia Muheza mjini katika kata ya Mbaramo hivyo basi kupelekea majengo ya taasisi ya awali kubaki wazi.
Akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa taasisi ya awali NIMR baada ya ukaguzi wa majengo vyo Ndugulile amesema majengo yote na ameyaona yanafaayako hivyo basi atakwenda kuzungumza na mhe waziri kwa ajili ya utekelezaji wa ombi la kuruhusiwa majengo hayo kuwa chuo kikuu. Pia alimtaka Mkurugenzi wa taasisi hiyo Ndugu wiliam Kisinza amkabidhi taarifa za mradi. Aliendelea kushauri kuwa taratibu cha kuanzisha chuo zikikamilika kiwe chuo kishiriki kinachotoa kozi za muda mfupi na waongeze idadi ya kozi kama vile kozi za mazingira, na misitu.
Akiendelea na Ziara yake katika Zahanati ya Ubwari na chuo cha vector control training centre Faustine alimuagiza mganga mkuu wa Wilaya (DMO) kuhakikisha taratibu za uandishi wa majina ya dawa kwa siri unafuatwa, na wasitumie madaftari kujaza taarifa za wagonjwa bali watumie patient note.
Kwa upande alipewa taarifa za walimu wanaojitolewa katika chuo cha vector control centre ili aweze kuwafanyia taratibu za kuajiriwa kwani chuo kina upungufu wa walimu na wao wanaonekana wana sifa ya kufundisha muda mrefu chuoni hapo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.