Naibu Waziri Ofisi ya Raisi TAMISEMI Mhe. Joseph George Kakunda amempongeza Mhandisi Joseph Kahoza kwa matengenezo ya barabara ya Kilomita 6 ya Mpapayu-Mgome kwa kufikia asilimia 75 ya matengenezo.
Mhe. Kakunda ameyasema hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Wilayani Muheza Agosti 15, 2018. Pia aliongeza kuwa mhandisi anafanya vizuri, hivyo basi anatakiwa kuwezeshwa ili amalize kazi yake kikamilifu kwani lengo la Serikali ni kuzipandisha hadhi barabara za mijini na vijjijini na kuwahudumia wananchi kwa ukaribu zaidi. Vilevile aliahidi kuongeza bajeti ya matengenezo ya barabara ili kuwe na barabara nyingi za changarawe na hatimaye rami.
Akisoma taarifa ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na 2018/2019 Mhandisi Joseph Kahoza alifafanua kuwa mpaka sasa matengenezo ya barabara hiyo yamefikia asilimia 75 ambapo kiasi cha Milioni 12 (Milioni kumi na mbili) zimetumika.
Pia aliongeza kuwa katika mpango wa mwaka wa Fedha 2018/2019 kiasi cha Takribani Bilioni 1.2 (1,268,950,000) zimeidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za matengenezo ya barabara za vijijini na mjini.
Aidha, Mhandisi alikumbushia maombi maalum ya barabara zilizoombewa kupandishwa hadhi kutoka barabara za Wilaya kuwa za Mkoa ambazo ni Kibaoni/Amani-Bulwa-Zirai KM 30, Kimbo-Potwe-Shambakapori km 16 na Kilulu-Mtindiro-Kwabada-Kwafungo km 40 kutokana na umuhimu wake wa kuiunganisha Wilaya ya Muheza na Wilaya za Mkinga na Korogwe.
Nae Ndugu Ismail Hassan mkazi wa Mpapayu amempongeza Mhandisi kwa matengenezo mazuri ya barabara na ameomba barabara iwekwe changarawe kwani barabara za udongo ni za msimu wa kiangazi na ikifika msimu wa mvua hazipitiki na hivyo kupelekea kushindwa kusafirisha mazao yao.
Akiendelea kutembelea miradi mingine Mhe. Kakunda amesisitiza utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ubora uliokusudiwa na kumalizika kwa miradi hiyo kwa wakati. Pia amesisitiza usimamizi sahihi wa fedha za miradi ya maendeleo na kuzingatia vigezo katika upatikanaji wa wakandarasi wenye uwezo.
Katika miradi iliyotembelewa, mradi wa maji Pongwe-Kitisa Muheza unatarajiwa kunufaisha watu 15,500 kwa kupata maji safi na salama kutoka asilimia 35 hadi asilimia 64, mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Mkuzi unaotarajiwa kumalizika Septemba 15, 2018 na mradi wa ujenzi wa vyumba vinne(4) vya madarasa , mabweni mawili(2) ya wanafunzi 160 ya shule ya sekondari Muheza (Muheza High School) hatua iliyofikia mpaka sasa ni kuchimba msingi kwa kutumia nguvu za wananchi na Serikali imeahidi kutoa kiasi cha Tsh. Milioni 230 kwaajili ya kutekeleza mradi huo.
Mradi wa maji Pongwe-Kitisa Muheza |
||
|
|
|
Mhe. Kakunda akisaini kitabu cha wageni katika eneo la ujenzi wa tanki la maji Kilapula
|
|
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tanki la maji Kilapula
|
Mradi wa wa ujenzi wa jengo la mama na watoto kituo cha afya Mkuzi |
||
|
|
|
Mhe Kakunda akisomewa taarifa ya mradi wa ujenzi wa jengo la mama na watoto kituo cha afya Mkuzi na kaimu Mganga Mkuu Ndugu Julius Mgeni.
|
|
Mhe Kakunda akikagua ujenzi wa jengo la mama na watoto kituo cha afya Mkuzi
|
Mradi wa ujenzi wa majengo ya Sekondari Muheza |
||
|
|
|
Naibu Waziri (wakwanza kulia) akikagua Ujenzi wa Sekondari Muheza
|
|
Naibu Waziri Kakunda akitoa maagizo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo sekondari Muheza
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.