Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe,Mwita Waitara amefanya ukaguzi katika miradi ya maendeleo ya Elimu, kwa upande wa shule ya msingi Pangamlima amekagua ujenzi wa darasa ilioingiziwa kiasi cha shilingi mil 7 ambazo zilitoka katika mradi wa EP4R( Motisha). Waziri amepongeza uwiano wa madawati na wanafunzi kuwa uko vizuri kwani darasa limejengwa vizuri kwakua linapitisha hewa ya kutosha.
Hata hivyo Naibu Waziri amewaasa Wanafunzi Kusoma kwa Juhudi na maarifa ili waweze kufikia malengo ya kuwawezesha kuzisaidia familia zao na Taifa kwa ujumla .Pia amewataka wazazi kuchangia kuwawezesha wanafunzi kupata mahitaji yatakayowawezesha wanafunzi hao kufanya vizuri darasani mfano, uwepo wa chakula shuleni na madaftari pamoja na vifaa vingine vya ziada vya kujifunzia .
Akiongea na wanafunzi na wazazi na wananchi na watumishi katika Shule ya Sekondari Songa Mh.Waitara alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na DR John Pombe Magufuli ipo katika mchakato wa kumalizia maboma yote( miradi viporo) yaliyotumia nguvu za wananchi ili huduma iliyokusudiwa kupatikana kupitia ukamilishaji wa majengo hayo uweze kupatikana kwa haraka. Hii itawawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati uliokusudiwa, hata hivyo wananchi wamepongeza serikali kwa kutoa kiasi cha tsh mil 100 ambacho kiliripotiwa kupokelewa mnamo tarehe 19/01/2019 ili kukamilisha ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Songa, Wananchi hao pamoja na wanafunzi wamempongeza mhe, Rais kwa jitihada zake za dhati katika kuwahudumia wananchi
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.