Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe, Dkt Mary Mwanjele amewatembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF waliopo katika kata ya Mkuzi jana Tarehe 13/2/2019 ili kujiridhisha na huduma itolewayo na waratibu wa TASAF waliopo Wilayani humo.
Akizungumza katika ofisi ya mkuu wa Wilaya muheza Mwanjele amesema lengo la Ziara yake ni kuangalia kama mradi wa TASAF una manufaa kwa walengwa kasha kuongea na watumishi wa umma ili kujua kero na changamoto zinazowakumba watumishi waliopo wilayani humo.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza aliwaasa kuvaa mavazi ya heshima , kufuata kanuni na taratibu za kazi kwani ndio utumishi wa umma unavyotaka na atakaekwenda kinyumea na taratibu ya mavazi ya utumishi achukuliwe hatua za kinidhamu.
Akisoma taarifa ya mradi Mratibu wa TASAF Wilaya Muheza Bi. Magdalena Kimaro amesema Mfuko wa maendeleo ya Jamii TASAF 111 Ulizinduliwa rasmi mwezi oktoba 2014 na unatekelezwa kwenye vijiji 90 kati ya vijiji 135 ambapo jumla ya kaya 6,800 zimebaki kwenye mpango.
Akiendelea kusoma taarifa hiyo Kimaro amlisema mpaka sasa malipo kwa kaya maskini yamefanyika kwa awamu 21 ambapo kiasi cha TZS. 4,759,470,800 kilipokelewa , kiasi kilicholipwa walengwa ni TZS4,163084744, na TZS 425,742,846 kimetumika kusaidia gharama za kuratibu ,kusimamia na kufuatilia uhawilishaji wa fedha kwa ngazi zote za Halmashauri, kata TZS. 44,002,433 pamoja na ngazi ya kijiji TZS. 135,209,521.
Nao wananchi wa kijiji cha MKUZI Wametoa pongezi kwa Serikali ya waamu ya tano inayoongozwa na DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI kwa kuanzisha mradi wa kunusuru kaya maskini kwani kupitia mradi huu wameweza kuwasomesha watoto na kuwanunulia vifaa vya shule, kuwapatia huduma za afya kama kuwapeleka kliniki na kununua mavazi ili kustiri miili yao.
Waliongeza kuwa mradi huu umewasaidia kukunua bati na kujenga nyuma na kufuga kuku na mbuzi hali inayopelekea kuongeza kipato cha kaya na kuishi katika nyumba bora hatimaye wameahidi kumuombea katika sala zao mhe Rais ili aendelee kuwasaidi katika maisha yao ya kila siku.
Mhe, Mary Mwanjelwa akizungumza na wanufaika wa TASAF Mkuzi. | Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza wakisikiliza maelekezo ya serikali yaliyokuwa yakitolewa na Naibu | |
|
||
Naibu Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndugu Mary Mwajelwa akizungumza na wanufaika wa TASAF jana katika ofisi ya kijiji cha mkuzi. |
|
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya MUheza wakisikiliza maelekezo ya kiserikali aliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri jana katika ujkumbi wa Mikutano wa Halmashauri. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.