Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imezindua mfumo wa Anwani za Makazi uliofanyika siku ya jumamosi tarehe 5/2/2022 katika kitongoji cha Tanganyika, kata ya Tanganyika Wilayani humo ambapo Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe. Halima Bulembo alikuwa Mgeni rasmi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo amesema zoezi hilo lina manufaa makubwa katika jamii yetu kwa kuwa itarahisisha upatikanaji wa mtu kwa haraka, ziaimarisha ulinzi na usalama wa mahali husika, na kuwezesha kufanyika kwa biashara mtandao.
Vilevile amewataka wananchi kutoa ushirikiana kwa wataalam watakaofika na kuweka namba kwenye nyumba na maeneo yao ili kuweza kufanikisha zoezi hili;
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza ambaye pia ni Afisa nyuki wa Wilaya hiyo Issa Msumari amesema zoezi hilo ni muhimu sana kwa kuwa litasaidia uwekji majina ya barabara na uboreshaji wa miundombinu hiyo.
Akielezea namna Muheza ilivyojipanga katika zoezi la Anwani za Makazi Msumari amesema zoezi hilo litafanyika katika kata 37, vijiji 126 na vitongoji 494 vilivyopo katika Wilaya hiyo.
Awali akisoma taarifa ya zoezi la Uwekaji Anwani za Makazi Mratibu wa zoezi hilo MKUMBO LEVI NGOI amesema Anwani za Makazi ni Utambulisho wa mahali/ mtu /kitu kilipo juu ya uso wa Nchi yenye lengo la kuharakisha upataji na utoaji na upelekaji wa huduma na bidhaa hadi mahali stahiki.
Aliendelea kuwa Wilaya ya Muheza ilianza kutekeleza zoezi hili rasmi kuanzia tarhe 24/01/2022 na linatarajiwa kukamilika mnamo tarehe 25/05/2022, ambapo mpaka sasa shughuli zilizokwisha kufanyika ni kutoa mrejesho ya semina wezeshi kwa kamati ya wataalam (CMT), kuwajengea uwezo watendaji wa kata 37 na wa vijiji 126ikiwa ni pamoja na kuainisha majina ya barabara na mitaa.
Aidha, Zoezi la Anwani za Makazi linatekelezwa nchi nzima ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Posta ya Mwaka 2003; makubaliano ya kimataifa (Pan African Postal union (PAPU) na Universal Postal Union (UPU) na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020-2025 kifungu Na. 61(m).
Mkuu wa Wilya Muheza akizindua zoezi la anwani za makazi | Mwenyekiti kamati ya anwani za makazi Thomas Mkwavi akielekeza jambo mara baada ya uzinduzi |
`
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.