Maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki yanahusisha Mikoa Minne ya Pwani, Dares- salaam, Tanga na Wenyeji Morogoro ambayo hufanyika kuanzia Agosti 1 hadi 8 ya kila Mwaka katika Viwanja vya Julius Nyerere Mkoani Morogoro.
Kaulimbiu ya maonesho ya nanenane kwa Mwaka huu wa 2022, inasema “Agenda 10/30 Kilimo ni biashara; Shiriki kuhesabiwa kwa Mipango bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi” kaulimbiu hii in lengo kusisitiza watu kujitokeza katika Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu ili kuisaidia Serikali kupanga Mipango ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Katika Maonesho haya mashindano hufanyika Kikanda na Kimikoa ikiwa lengo ni kuleta Motisha katika shughuli za kilimo, Mifugo na Uvuvi zilizopo kwenye Mikoa na Halmashauri kwa ujumla ili kuweza kuleta tija katika sekta hizo.
Kwenye Mashindano ya kuushindanisha Mkoa wa Tanga katika Halmashauri zake zote 11, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imeshika nafasi ya tatu baada ya nafasi ya kwanza kushikwa na Tanga jiji, na Halmashauri ya Lushoto ikishika nafasi ya Pili.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusheherekea ushindi iliyofanyika Mkoani Morogoro iliyohusisha Waheshimiwa madiwani wa kamati ya fedha, Wakuu wa idara na vitengo na wataalam wa kilimo na Mifugo, Katibu Tawala Wilaya Muheza Desderia Haule alisema ushindi huo umetokana na juhudi nyingi zilizofanywa na wataalam na ubunifu uliofanyika wa kurekodi sauti iliyokuwa ikitoa elimu juuu ya namna bora ya upandaji wa Mazao ya viungo ambayo ilisikika muda wote pindi watu wapitapo katika eneo la banda la Muheza.
Pia amekiopongeza kikundi cha wajasiriamali ‘MBOMOLE HILL SPICE FARMERS GROUP’ kilichopo katika kata ya Mbomole tarafa ya Amani kwa kuleta bidhaa nzuri za Mazao ya viungo zilizosindikwa na zisizosindikwa katika banda hilo.
Aidha katika nane nane ya Mwaka huu wa 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Muheza katika Banda lake kumezalishwa Mbogambaga za Mchicha, Spinachi, Mnavu ,na Bamia, Matunda aina ya machungwa, bidhaa zilizosindikwa za mazao ya viungo na visivyosindikwa, Mifugo ya kuku vilikuwepo katika banda hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe, Jerome Mhina amesema atahakikisha Halmashauri inatenga bajeti ya kutosha katika maonesho ya nanenane ya Mwaka ujao wa 2023 ili waweze kushika nafasi ya juu Zaidi lakini pia alsisitiza kuwa sherehe hizi hzi zisiishie kwenye kanda pekee bali zifanyike mpaka kwenye Wilaya ili kuasaidia wakulima waweze kujifunza teknolojia mpya za kilimo na Mifugo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.