Maonesho ya nane nane, 2022 kanda ya Mashariki yanajumuisha Mikoa ya Dar-es-Salaam, Pwani Tanga na Morogoro ambayo hufanyika kila Mwaka kuanzia Agosti 1-8 katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Mkoani Morogoro.
Kaulimbiu ya Mwaka huu wa 2022 inasema “Agenda 10/30 kilimo ni biashara ; Shiriki kuhesabiwa kwa Mipango bora ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ni miongoni mwa Halmashauri 11 zinazounda Mkoa wa Tanga ambazo hushiriki kikamilifu katika maonesho ya nane nane kanda ya mashariki.
Wilaya ya Muheza imejipanga kwa kufanya maandalizi katika banda lake kwa kkufanya usafi wan je na ndani
Pia wameanza kufyeka, na kulima eneo la bustani ya mboga mboga (vipando) ili kuhakikisha miche itakayopandwa inakuwa katika sehemu safi na yenye kupendeza kwa ajili ya ukuaji mzuri na ubora wa mazao hayo.
Vile vile ukarabati wa banda na Mbuzi, na ngombe unafanyika kikamilifu kuhakikisha wanyama watakaoletwa wankaa mahali pazuri na salama kwa afya yao.
Kwa kuwa muda wa kuanza vipando umesogea sana Afisa Kilimo Wilaya ya Muheza Ndugu Hoyange Marika Mbwambo na Afisa Mifugo ya Wilaya hiyo Dkt Edward Mgaya wameshauri zipandwe mbogamboga za muda mfupi kama vile Mnavu, Mchicha, Spinachi, Sukuma wiki, na bamia.
Aidha Maonesho hayo yatahusisha uletwaji wa bidhaa mbalimbali za mazao yanayolimwa Muheza kama vile, Machungwa, mazao ya viungo mdalasini , iriki karafuu mabvyo mara nyingi husindikwa na wajasiramlai wa Wilaya hiyo.
|
|
|
Ukarabati wa banda la kuku unaendelea katika eneo la banda la Muheza | Afisa kilimo Wilaya ya Muheza Hoyange Marika kushoto akijadili jambo na Afisa Mifugo na Uvuvi Edward Mgaya mwenye shati jeupe mara baada ya kukagua eneo la vipando vya Muheza katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Mkoani MOROGORO tarehe 29/6/2022 | Aifisa Mifugo Wilaya ya Muheza Edward Mgaya na Hoyange Marika afisa kilimo wa Wilaya hiyo wakielekea kwenye kikao cha maandalizi ya nane nane uliofanyika tarehe 29/6/2022 katika ukumbi wa JKT nanenane mara baada ya kukagua banda la maonesho la Wilaya yao. |
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.