• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Muheza District Council
Muheza District Council

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Ugavi na Manunuzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Utalii
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa Kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya AFYA
    • Kilimo
    • Elimu
    • Ardhi
    • TEHAMA
      • Huduma
      • Mifumo
        • PLANREP
        • FFARS
        • PREM
        • Salary Slip Portal
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha

MUHEZA YAJIPANGA KUANZA ZOEZI LA SENSA

Posted on: January 19th, 2022


Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imejipanga kikamilifu kuanza zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika mnamo Mwezi Agosti 2022 ikiwa na lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya Makazi.

Akizungumza katika kikao cha kwanza cha kamati ya Sensa Wilaya,kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Abdallah Bulembo ambaye ni Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa kamati hiyo amesema akiwa katika ziara yake ya kutembelea vijiji zenye lengo la kutatua kero za wananchi amekuwa akisisitiza jamii kuhesabiwa katika zoezi la sensa.

Vile vile ameitaka jamii kuepukana na dhana potofu ya kuficha makundi maalum yaani watu wenye ulemavu wakati wa zoezi hili  wawaache wahesabiwe na  kuingizwa kwenye mipango ya Serikali ili waweze kupatiwa misaada wanayohitaji.

Awali akisoma taarifa ya Maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022 ya Wilaya ya Muheza Mratibu wa Sensa Wilaya ambaye pia ni Afisa takwimu wa Wilaya hiyo Nelson Mwankina amesema mpaka sasa kamati moja ya Wilaya, 37 za kata na kamati 126 za vijijizimeundwa kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na TAMISEMI.

Aliongeza kuwa maeneo ya kuhesabia yameshatengwa na kuhakikiwa na wataalam kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Viongozi wa Maeneo husika ambapo hadi kufikia tarehe 31/12/2021 kata 37, Vijiji 126 na Vitongoji 494 vimepitiwa na kuhakikiwa mipaka yake.

Aliendelea kuwa shughuli zitakazoendelea kufanyika ni uhamasishaji wa wananchi kupitia mikutano mbalimbali ngazi ya  Wilaya mpaka Vitongoji pamoja na kutumia viongozi wa dini (waislam na wakristo, Walimu wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari,Mashirika yasiyo ya kiserikali, Maafisa tarafa na Sherehe mbalimbali za kitaifa.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya takwimu Makao Makuu DODOMA Bi. Zawadi Salehe Chanzi amezitaja baadhi ya faida za sensa kwamba husaidia kupanga maendeleo ya nchi kama vile kujenga Shule, Vituo vya kutolea huduma za afya na huduma mbalimbali jamii na kusisaidia Serikali kutatua changamoto za ardhi katika maeneo husika.

Tangazo

  • WANAOITWA KWENYE USAILI NAFASI ZA KAZI ZA AFYA October 12, 2024
  • MATOKEA YA NAFASI ZA UDEREVA October 10, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI VIJIJI, MADEREVA NA MWANDISHI MWENDESHA OFISI October 25, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI VIJIJI, MADEREVA NA MWANDISHI MWENDESHA OFISI October 25, 2024
  • Angalia Vyote

Habari mpya

  • RAIS SAMIA AKOSWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI MAGILA AMRUHUSU AKAE KWENYE KITI CHAKE CHA RAIS

    February 28, 2025
  • RAIS SAMIA AKOSWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI MAGILA AMRUHUSU AKAE KWENYE KITI CHAKE CHA RAIS

    February 28, 2025
  • RAIS SAMIA AKOSWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI MAGILA AMRUHUSU AKAE KWENYE KITI CHAKE CHA RAIS

    February 28, 2025
  • MICHAEL MSECHU AONGOZA WANANCHI WA MUHEZA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA

    February 19, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Mhe. Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania akizindua uchangiaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sheria Ndogo za Halmashauri
  • Ratiba ya vikao vya kisheria
  • Video za Matukio Mbalimbali
  • Huduma za Afya zinazopatikana
  • Mpango Kazi wa Halmashauri
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani na Taarifa za Kata
  • Mawasiliano ya Walimu wakuu wa Shule za Msingi na sekondari

Viunganishi linganifu

  • Ikulu
  • Mbinu mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi , Milma ya Usambara Mashariki, Muheza.
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Idara kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Muheza Mjini, Bomani

    Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA

    Simu: 027-2977545

    Simu ya Mkononi: 0746525653

    Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.